Mkurugenzi Mtendaji H/W Chunya Bi. Sophia Kumbuli akichangia hoja katika kikao hicho, Mbele yake ni M/kiti wa Halmashauri ya Chunya Mh. Bosco Mwanginde akisikiliza kwa makini.
Mbeya.
OR-TAMISEMI Kupitia fedha za wadau wa Maendeleo inatekeleza miradi ya ukarabati wa vituo vya Afya nchini kwa ajili ya
kuviwezesha kutoa huduma za uzazi za dharura (CEMONC). Awamu ya kwanza ya ukarabati ilianza mwezi Oktoba 2017 ambayo
ilihusisha vituo vya afya 44 katika Halmashauri 43 na kati ya vituo hivyo Mkoa wa Mbeya ulikuwa na vituo vya afya viwili
ambavyo ni “Kituo cha afya Ipinda (Kyela)” na “Kituo cha afya Ikuti ( Rungwe)”
Katika kutekeleza Miradi hiyo utaratibu wa “Force Account” umekubalika kutumika ambapo Halamshauri husika kwa kushirikiana
na Secretariet ya Mkoa wanapaswa kusimamia kwa ukaribu kazi zinazofanyika katika maeneo ya miradi ili kuhakikisha
kunakuwa na ubora katika vituo vilivyokarabatiwa/kujengwa
Awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi imeanza tarege 02/01/2018 na inatarajiwa kukamilika 30/04/2018. Mkoa wa Mbeya
umekwisha pokea fedha jumla ya Shilingi 3,000,000,000.00(Bilioni tatu) kwa ajili ya ukarabati/Ujenzi wa vituo vya Afya
sita katika Halmashauri za Chunya (1), Mbeya DC(3 ) na Busokelo (1),
Katika kutekeleza hili, Halmashauri Wilaya ya Chunya imeshaanza ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chalangwa kata ya
Chalangawa.
Zifuatazo baadhi ya picha zikionesha hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi huo katika Halmashauri ya wilaya ya
Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.