Mkuu wilaya ya Chunya, Mh.Maryprisca Mahundi amegawa na kuwasainisha Maafisa watendaji wa kata na vijiji mikataba kwa ajili ya utekelezaji wa ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo wadogo.
Zoezi la usainishaji wa mikataba limefanyika katika ukumbi wa halmashauri (SAPANJO HALL) kwenye kikao cha Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi, wakuu wa idara na vitengo watendaji wa kata na vijiji chenye lengo la kufanikisha ugawaji wa vitambulisho kwa kila mjasiriamali mdogo mwenye mtaji usiozidi Tsh 4,000,000/= kwa mwaka.
Mahundi amesema kuwa kila mtu anatakiwa kujua kuwa anawajibu mkubwa wa kutekeleza agizo la mweshimiwa Rais, hivyo mbali na kuwa na majukumu yao ya kila siku suala la ugawaji wa vitambulisho lipewe kipaumbele.
"Ukiwa kama mtumishi wa serikali busara itumike, sitaki urasimu katika zoezi la ugawaji, ugawaji wa vitambulisho uwe kwa watu wote wanaostahili, iwe mkulima, bodaboda, mpiga debe na wengine wote.” Mahundi.
Halmashauri ya wilaya ya Chunya ilipewa jumla ya vitambulisho 5000 kwa awanu ya kwanza, pia 5000 awamu ya pili. Vitambulisho 1200 vimegawiwa na kubakiwa na vitambulisho zaidi ya 8000 vinavyotakiwa kugawiwa kwa wajasiliamali wadogo wadogo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.