Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kukataa wagombea wote watakaokuwa na lengo la kuwagawa na kueneza chuki kwa wananchi wa wilaya ya Chunya bali kupitia uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 wananchi wa Chunya waungane ili waweze kuchagua viongozi wazuri watakaomsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania wakiwepo wananchi wa wilaya ya Chunya
Akizungmza mapema leo tarehe 5/10/2024 katika mikutano tofauti tofauti aliyoifanya Kitongoji cha Ilindi kata ya Matwiga, Kitongoji cha Tulieni na Kitongoji cha Mafyeko vilivyopo kata ya Mafyeko ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki kujiandikisha na hatimaye kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa mapema mwezi Novemba, amesema uchaguzi unaotaraji kufanyika uwaunganishe wananchi ili kwa pamoja wachague viongozi wazuri wataowaletea maendeleo huku akionya watu wanaokusudia kuleta mgawanyiko
“Msiwapokee wagombea wanaokuja kwa lengo la kuleta mgawanyiko, Maana yake hawana makusudi mema kwenu. Na ni matumaini yangu Uchaguzi wetu sisi Chunya utakuwa wa Mfano watu watakuja Chunya kujifunza namna ambavyo wananchi wameshiriki uchaguzi kwa Amani kabisa” Amesema Mhe. Batenga
Aidha Mhe Batenga amewakumbusha wananchi wa Chunya umuhimu wa Amani katika wilaya ya Chunya huku akiwakumbusha wananchi kwamba wanafanya shughuli zao kwa Amani, wanaweza kusafiriki kutoka eneo moja kwenda eneo lingine bila usumbufu wowote kwasababu wananchi pamoja na viongozi wao wanashirikiana kuhakikisha amani hiyo inalindwa hivyo amewataka wananchi waendelee kuwa watulivu ili nchi ya Tanzania iendelee kuwa na Amani
Pamoja na Elimu hiyo kuelekea Uchaguzi Mhe. Batenga ameendelea kusikiliza kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi huku akiwaambia wananchi kwamba Serikali ya awamu ya sita ni ya ukweli na uwazi jambo linalofanya wakati wote ajibu hoja za wananchi wake kwa ukweli na uwazi
Wananchi wa Ilindi, Tulieni na Mafyeko wameshukuru ziara ya Mkuu wa wilaya kufika katika maeneo yao huku wakikili wazi kwamba ni ziara ya kwanza kwa kiongozi mkubwa katika wilaya ya Chunya kufanya ziara katika baadhi ya vitongoji mbalimbali vya wilaya ya Chunya ikiwa ni pamoja na Tulieni na ilindi
Mkuu wa wilaya ya Chunya ameanza Ziara ya Siku tatu yenye lengo la kuhimiza wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha wanajitokeza kushirki uchaguzi kwa kuanza na kujiandikisha, kugombea na hatimaye kushiriki kupiga kura tarehe kwenye uchaguzi unaotaraji kufanyika Novemba 27, 2024 ambapo wananchi wanapaswa kujiandikisha katika vitongoji wanavyoishi na vituo hivyo ndipo wananchi watakapoenda kupiga kura
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.