Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya anapenda kuwajulisha kuwa tume ya Uchaguzi itaanza kutekeleza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga Kura katika Wilaya ya Chunya kuanzia tarehe 17/12/2019 ambapo Vituo vya Uboreshaji vilivyopo katika Kata zote 20 za Wilaya ya Chunya vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni kila siku.
Walengwa wa zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni wafuatao:-
i/. Raia wote wa Tanzania waliotimiza umri wa miaka 18, lakini hawajawahi kujiandikisha, yaani hawakuwahi kuwa na kitambulisho cha Mpiga Kura cha 2015
ii/. Raia wote wa Tanzania watakaotimiza umri wa miaka 18 ifikapo tarehe 22 Oktoba 2020 au kabla ya hapo.
iii/. Wale wote waliowahi kujiandikisha na kupewa kadi ya Mpiga Kura , lakini kwa sababu moja ama nyingine wanahitaji kupewa kadi mpya kutokana na mojawapo ya sababu zifuatazo
A) Kadi husika kupotea, au
B) kadi husika kuharibika, na au
C) Mhusika amebadilisha makazi kutoka kata, Wilaya na Mkoa mmoja kwenda mwingine.
D) Mhusika anaboresha tarehe, jina,umri au jinsia kama ilikosewa.
Kwa hiyo, Wananchi wote wa wilaya ya Chunya mnaombwa kujitokeza kushiriki zoezi hili muhimu ndani ya muda huu mfupi uliopangwa.
NB: WANANCHI AMBAO TAARIFA ZAO ZIPO SAHIHI NA HAWAJAHAMA MAENEO YAO WALIYOANDIKISHWA MWAKA 2015 HAWANA HAJA YA KUJITOKEZA KATIKA UBORESHAJI HUU HIVYO WANAASWA KUJIANDAA NA UCHAGUZI WA MWAKA 2020.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.