Zaidi ya asilimia 80 ya shule za msingi na sekondari wilayani Chunya zinatoa Chakula Cha Mchana kwa wanafunzi ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha suala la lishe linazingatiwa wilayani Chunya huku asilimia zilizosalia kukakamilika ifikapo Julai 2023.
Akitoa taarifa za utekelezaji wa Afua za lishe kwenye kikao cha Lishe wilaya ya Chunya Kaimu Afisa Lishe Bi. Witness Kisukulu, amesema Chunya sasa asilimia 85 ya shule zote wilayani Chunya Hutoa Chakula ambapo kupitia kikao hicho kilichoongozwa na Afisa Utumishi wa wilaya ya Bw John F. Mohalani akimuwakilisha Mkurugenzi mtendaji, Wameazimia ifikapo Julai mwaka huu wilaya ifikishe asilimia 100 katika utoaji wa Chakula shuleni
Katika kufikia kiwango cha asilimia mia moja sheria ndogo ndogo za halmashauri zipo katika hatua mbalimbali za maandalizi ambazo zitatumika kuwabana wazazi ambao hawatatoa ushirikiano kuchangia chakula ili wanafunzi wawapo shuleni wapate chakula cha Mchana
Aidha Katibu wa kikao hicho ambaye ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya Dr. Darison Andrew amewaomba wajumbe wa kikao hicho kuongeza juhudi sana katika kusimamia suala la lishe ambapo amesema gharama za kumhudumia moto mwenye utapiamlo ni kubwa sana huku akiwaahidi kuhakikisha usafiri unapatikana ili kuwafikia wananchi wote wa wilaya ya CHUNYA
Kikao hicho cha Robo ya tatu ya mwaka 2022/2023 kimeketi leo Tarehe 3, 2022 katika ukumbi wa mikutano uliopo jengo jipya la utawala kimeongozwa na Afisa utumishi wa wilaya ya Chunya Bw JOHN F. Maholani akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Chunya Ndugu, Tamimu Kambona
Katibu wa kikao cha Lishe ambaye ni Mganga Mkuu wa wilaya Dr Darison Andrew akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kikao
Mwenyekiti wa Kikao cha Lishe wilaya ya Chunya Bw. John Maholani akihitimisha kikao hicho na kuwataka wajumbe kutekeleza makubaliano ya kikao
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.