Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Tamim Kambona amewataka viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wilaya ya Chunya kuhakikisha wanazingatia ratiba ya Kampeni huku akiwataka kuwasilisha maboresho ya ratiba hiyo saa yoyote inapohitajika ili kikao cha maridhiano kuhusu maboresho hayo kifanyike na kampeni kuendelea kama ilivyopangwa
Akizungumza mapema tarehe 19/11/2024 kwenye kikao kilichohusisha viongozi wa vyama vya siasa vyote vinavyotaraji kushiriki Uchaguzi pamoja na viongozi wa vyomba vya Usalama, Kambona amewashukuru viongozi wa Vyama vya siasa kwa ushirikiano wanao utoa kwake katika kuhakikisha Halmashauri ya wilaya ya Chunya inafanya Uchaguzi huru, shirikishi na wenye kufua Sheria, taratibu na miongozo ya Uchaguzi jambo litakalopelekea Chunya kuigwa katika Taifa hili la Tanzania
“Mabadiriko haya ya ratiba yataendelea kufanyika mara kwa mara kulingana na mapendekezo yenu ninyi viongozi wa vyama vya siasa wakati mnaendelea na Kampeni na wakati wowote mnapoona kero yoyote wasilisheni kwangu ili ifanyiwe kazi kwa wakati, Aidha niwashukuru sana viongozi wa Vyama vya siasa kwa namna tunashirikiana tangu tulipoanza maandalizi yote ya Uchaguzi na pia tuendelee kushirkiana mpaka tunakamilisha uchaguzi wetu tarehe 27/11/2024” Alisema Kambona
Naye Afisa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Ridhiwan Mshigati amewashukuru viongozi wa vyama vya siasa kwa ushiriki wao lakini pia amewakumbusha kutumia njia sahihi zinazoelezwa kwenye Sheria pindi wanapokuatana na Changamoto ili kuleta suluhu wa Changamoto iliyojitokeza wakati wa Michakato mbalimbali ya Uchaguzi inayoendelea
Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Chunya Ndugu David Kambona pamoja na mambo mengine aliyoelekeza wakati wa kikao hicho, aliwakumbusha viongozi wa vyama vya siasa na wajumbe wa wa kikao kwa ujumla kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni za Uchaguzi huku akiwakumbusha kosa la Rushwa ambalo mara nyingi hujirudia katika mambo ya Uchaguzi
“Mojawapo ya makosa ambayo hufanyika mara kwa mara ni kosa la Rushwa, ni kosa kutoa fedha au zawadi kutoka kwa wagombea, kununua kura au kutoa malipo yoyote kwa mpigakura, msimamizi wa kituo nalo ni kosa, kubeba au kusafirisha wapiga kura kwaajili ya kwenda kupiga kura pia ni kosa hivyo niwaombe tuzingatie sheria za Uchaguzi” Alisema Kambona
Naye Mkuu wa Polisi wilaya ya Chunya SSP Nestory John amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuwakumbusha wanachama wao kwamba Tanzania itaendelea kuwepo na hata wananchi wataendelea kuwepo hivyo ni vema wakatambua hili na kila jambo wafanye wakiwa wanajua maisha yataendelea
Kikao hicho kilihusisha viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Viongozi wa ACT-WAZALENDO, Viongozi CHAUMA pamoja na viongozi vya Vyombo vya Usalama wilaya ya Chunya huku lengo likiwa ni kufanya mapitio ya Mwisho wa Ratiba za Kampeni kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Mapema 27.11.2024
Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Chunya Ndugu David Kambona akiwasilisha mada wakati wa kikao cha Kufanya mapitia ya mwisho ya Ratiba ya Kampeni kilichofanyika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Chunya kikihusisha viongozi wa Vyama vyote vitakavyoshiriki Uchaguzi
Kamanda wa Polisi Chunya SSP Nestory John akiwasilisha mada ya Usalama wakati wa Kampeni na Uchaguzi kwenye kikao cha Viongozi wa Vyama vya siasa kilichoketi jana kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Chunya
DSO wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya akisisitiza Jambo wakati wa kikao na Viongozi wa Vyama vya siasa kuelekea Kampeni zinazoanza tarehe 20.11.2024
Afisa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Ridhiwan Mshigati akifafanua Jambo wakati wa kikao kilichoketi kikihusisha viongozi wa Vyama vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.