Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mayeka S Mayeka amewataka wananchi waliojenga, kuishi na kufanya shughuli mbalimbali kwenye njia za mapitio ya wanyama (Shoroba) na kwenye hifadhi ya misitu kutoka maeneo hayo kabla hawajaanza kuondolewa
Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa juma wakati alipokuwa akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika kijiji cha Bitimanyanga alipoongoza kamati ya ulinzi na usalama kusikiliza kero pamoja na kutembelea miradi itakayopitiwa na mwenge wa uhuru 2023 ambapo unatarajiwa kupokewa na kukimbizwa wilayani Chunya tarehe 13.09.2023
“Tokeni kwenye Shoroba na Misitu inayotunzwa na kuhifadhi Kisheria kwani misitu hiyo ipo Kisheria na zipo sheria ambazo zinaweza kupelekea mtu kufungwa kwasababu tu anaharibu mazingira, hivyo tokeni kabla hatujaanza kuwatoa”alisema Mhe.Mayeka
Aidha Mhe Mayeka amewataka wanachunya kuanza kuweka mipango bora ya ujenzi wa vijiji vyao ili kuhahakisha inapitika vizuri kuliko kusubiri utaratibu wa serikali ambao unaweza kuchukua muda mrefu kukamilika kuliko wanavyoweza kujisimamia wenyewe kupitia serikali za vijiji na kata kwenye maeneo wanayoishi
Meshack Furahisha, Julius Nguvumali na Janeth Haison wamewawakilisha wananchi wengine kutoa kero za maeneo yao ambazo zilijikita katika uchafuzi wa mazingira, kero za wafugaji kulisha mazao lakini pia wakulima kushindwa kulipwa fedha zao kutoka Kampuni ya Mkwawa jambo ambalo linaleta changamoto kwa maandalizi ya kilimo kwa msimu ujao
Kero zote zilipata majibu kutoka kwa Mkuu wa wilaya ambapo aliwataka wananchi kuwa wavumilivu kwani serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia inajali wananchi wake hivyo suala la malipo yao linafuatiliwa kwa ukaribu sana kuhakikisha wanalipwa fedha zao
Awali akitoa salamu za wananchi wa kata ya Mafyeko Diwani wa kata hiyo Mhe Geofrey Z. Kamaka alipongeza kamati ya usalama kukubali kupeleka mkesha wa Mwenge eneo la Biti manyanga na amesema wananchi wa Bitimanyanga watautendea haki mwenge wa uhuru kwa kukesha katika eneo la Mkesha kwa utulivu
Ziara hiyo ya kamati ya Usalama ilihitimishwa kwa kukagua eneo la mkesha wa Mwenge na kutoa ushauri zaidi wa maeneo ya kuboresha tayari kwa shughuli ya mwenge ambao utapokelewa tarehe 13/9/2023 katika uwanja wa Sinjilili na baadaye Mkesha utakuwa uwanja wa mpira wa Miguu Bitimanyanga.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.