Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Alhaji Batenga akimuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewapongeza wachezaji wa timu ya KENGOLD kwa kurudi nyumbani na Ushindi mkubwa na kuuheshimisha Mkoa wa Mbeya, akiongeza kuwa ombi lao la kukamilisha Uwanja wa michezo Wilaya ya Chunya uliopo kata ya Mbugani amelichukua ili mashindano mbalimbali ya kimkoa na kitaifa yaweze kufanyika katika uwanja huo.
Ametoa Kauli hiyo leo tarehe 09/05/2024 katika uwanja wa Mpira wa miguu Sinjilili akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika Mapokezi ya Timu ya Mpira wa Miguu ya KENGOLD iliyofanikiwa kutwaa kombe la Championship na kufanikiwa kupanda Ligi Kuu msimu ujao wa soka 2024/2025.
“Ombi lenu la kukamilika kwa uwanja nimelipokea na linafanyiwa kazi na niwaahidi uwanja wetu utakamilika , tunataka mashindano mbalimbali yafanyike katika viwanja vyetu , timu ya Simba na Yanga zije zicheze katika viwanja vyetu pamoja na mashindano mengine yakayokuwa yanafanyika katika ngazi mbalimbali “.amesema Mhe.Batenga
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Bosco mwanginde amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza kuchangia ujenzi wa uwanja unaojengwa katika kata ya mbugani ili timu mbalimbali ziweze kufika na kucheza katika uwanja huo kwani faida ya timu zinapokuja kucheza ni biashara lakini pia burudani kwasababu timu zinapocheza wafanyabiashara wanapata fursa ya kuuza bidhaa zao na kutoa huduma mbalimbali na hatimae kujipatia kipato .
“Chunya kama itakuja timu ya Simba au Yanga tunajua tunauhakika wa kufanya biashara kwani timu ni biashara na burudani kwahiyo nawaombeni sana wadau mliopo hapa tuchange michango yetu ili tukamilishe uwanja wetu kusudi timu mbalimbali ziweze kuja kucheza chunya mimi na Mkurugenzi wangu tayari tumetenga bajeti na tutasimamia kuhakikisha fedha zilizotengwa zinafanya kazi hiyo” amesema Mhe. Mwanginde
Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mbeya ndugu Lukas Kubaja pamoja na kuupongeza uongozi wa Chama cha Mpira wilaya ya Chunya, amewataka vijana wenye vipaji kujitokeza kujiunga na timu ya KENGOLD lakini pia amewataka watoto wakike nao wajitokeze na kujiunga na timu ya KENGOLD kwani timu hiyo imejipanga kuwa na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka ishirini lakini pia kuwa na timu ya kike ya mpira wa miguu.
Shamla shamla za mapokezi ya timu ya KENGOLD iliyoibuka na ushindi wa ligi daraja la kwanza zimepambwa na burudani mbalimbali huku kombe hilo likipitishwa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya huku viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakijitokeza kuilaki timu hiyo
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga akikabidhiwa Kombe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wakati wa Mapokezi ya Timu ya KENGOLD mapema leo kwenye uwanja wa mpira wa Miguu wa Sinjilili wilayani Chunya
Umati wa wananchi wa Chunya waliojitokeza kwenye uwanja wa Mpira wa Miguu Sinjilili Kuipokea timu yao ya KENGOLD baada ya kufanikiwa kutwaa kombe la Ligi daraja la Kwanza na hatimaye kufanikiwa kupanda Ligi Kuu kwa msimu ujao 2024/2025
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.