Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) nyanda za juu kusini imetoa mafunzo ya udhibiti na Usambazaji wa Mbolea kwa vyama vya ushirika wilayani chunya kwa lengo la kuhakikisha uduma ya mbolea bora inawafikia wakulima wote kwenye maeneo yao.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku mbili kuanzia April 12- 13, 2023 katika ukumbi wa halmashauri (Sapanjo) ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo mada juu ya matumizi sahihi ya mbolea, umuhimu wa kupima afya ya Udongo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Meneja wa TFRA kanda ya nyanda za juu kusini Ndugu Michael Sanga amewataka washiriki walio shiriki mafunzo hayo kwenda kuifikisha elimu waliyoipata kwa wananchi.
“Huo ujumbe ambao mmeupata nyinyi ndio ambao mnatakiwa kumpatia mkulima, mnawajibu wa kutoa elimu kwa wakulima wenzenu kwa kupitia biashara mtakayokuwa mnafanya sio tu kuwauzia mbolea” amesisitiza Sanga.
Naye Bw. Enricko Renatus mmoja wa wakufunzi katika mafunzo hayo ambaye ni Mdhibiti Ubora wa Mbolea Kanda ya nyanda za juu Kusini amesema lengo hasa la kutoa elimu kwa vyama vya ushirika ni kuhakikisha huduma ya mbolea bora inawafikia wakulima wote.
Aliongeza kusema wanaamini vyama vya ushirika vina wakulima wengi hivyo kwa elimu waliyo ipata watakwenda kuwafikishia, aidha vyama hivyo visaidie kusambaza mbolea kwa wakulima katika maeneo yao.
Kwaupande wa Afisa Kilimo, mifugo na Uvuvi wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Cuthbert Mwinuka amesema mafunzo hayo yametolewa kulingana na agizo la waziri wa Kilimo, mifugo na Uvumi Mhe Hussen Bashe la kutaka vyama vyote vya ushirika view mawakala wa kusambaza mbolea kwa wakulima
“Kwa kutekeleza agizo hilo tumetoa mafunzo ili wajue kanuni za kuuza mbolea na waitambue mbolea yenyewe ili waweze kufanya kazi yenye ufanisi Zaidi” amesema Mwinuka
Aidha Mwinuka amesema wilaya nzima sasa kutakuwa na mtandao wa kuanzisha uwakala wa kuuza mbolea kwa wananchi na mbolea itafika kwa wakati
Viongozi wa Vyama vya Ushirika wakiwa kwenye Mafunzo ya Udhibiti na Usambazaji wa Mbolea
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.