Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Suleiman Jafo, ameagiza mwekezaji yeyote asiruhusiwe kufanya Uchimbaji wa madini ndani ya Mto Zira mpaka pale wataalamu watakapo jiridhisha utunzaji wa Mazingira.
Mhe. Jafo ametoa kauli hiyo jana January 19, 2024 baada ya kufanya ziara ya kutembelea na kukagua kampuni ya G & I inayofanya shughuli za Ujichambaji wa madini katika Mto Zira unaopita kata ya Ifumbo kuelekea ziwa Rukwa
“Hawa wawekezaji wote hakuna mtu atakaye ruhusiwa kufanya uchimbaji humu lazima kwanza wataalamu wangu wa Mazingira wajiridhishe, kwamba wajiridhishe hilo jambo linawekezekana vipi na kuhakikisha mazingira yanalindwa”.
Mhe. Jafo amesema wawekezaji wote walipo kwenye ukanda wa Mto Zira wahakikishe wana kamilisha tathimini ya uharibifu wa Mazingira na amewataka Wataalamu tota ofisi yake kuhakikisha hiyo tathimini ya mazingira iwe na masharti mahususi yatakayo ainisha nini mwekezaji anapaswa kufanya
Pia Mhe. Jafo aliongeza kusema hatarajii kuona uchakataji wa madini unafanyika ndani ya Mto, shughuli zote zifanyike nje ya Mto na wataalamu waainisha ni umbali gani inafaa shughuli hizo kutafanyika
“Uchakataji wote akichukua Mchanga ufanyike nje ya Mto mtasema nyinyi ni umbali kiasi gani nyinyi ndio wataalamu, kwasababu kuna dhahabu nyingi na ni utajiri mkubwa hatuwezi tukaiacha hiyo dhahabu” Alisema Mhe. Jafo
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Z. Homera amesema ana amini kwenye teknolojia kwani tukiwekeza kwenye teknolojia tunaweza kuchimba dhahabu na maji yasichafuke lakini pia tutaepuka madhara yanaweza kujitokeza kutokana na kemikali zinazotumika wakati wa Uchenjuaji
“Tukienda kwenye Nchi za wenzetu huko wanateknolojia nyingi sana maji yanaweza yasichafuke na watu dhahabu wakaondoka nayo, kitu kikubwa nacho sisitiza hapa huyu mwekezaji awekeze kwenye teknolojia ili madini yaweze kutoka kwa maslahi mapana ya Nchi yetu” alisema Mhe. Homera
Katika ziara hiyo Mhe Jafo ametembelea kiwanda cha kuchenjua Dhahabu cha Anglo De Beers kilichopo kitongoji cha mwaoga kata ya Makongolosi wilayani Chunya na amewapongeza wawekezaji wa kiwanda hicho kwa uwekezaji mkubwa na kutengeneza ajira kwa watanzania.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Suleiman Jafo, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga na Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Z Homera wakiwa wanakagua uwekezaji kwenye uchimbaji wa dhahabu wilayani Chunya
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga aliyesimama akitoa taarifa Mbele ya Waziri Jaffo(Hayupo pichani) wakati alipotembelea wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.