WATAALAM toka Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na wataalamu toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya sambamba na wataalam kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Chunya, wamefanya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Dkt. Sonda Shabaan ambaye ni Msimamizi wa miradi ya afya kota Tamisemi ametoa pongezi kwa uongozi wa halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa Wilayani hapa.
“Tunawashukuru kwa usimamizi wa miradi, usimamizi mzuri ‘technical issues’ (masuala ya kiufundi) ni chache sana ukilinganisha na maeneo mengine tumepita,” alisema Sonda.
Aidha alipongeza ubora wa majengo, ushirikiano baina yao na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
Pia Dkt. Sonda ameutaka uongozi wa halmashauri kuhakikisha unatatua changamoto zote zinazojitokeza kwenye miradi hiyo ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa maji ili miradi hiyo inapokamilika wananchi waweze kufaidi huduma hiyo ya muhimu kwa jamii.
“Kituo hiki cha Mafyeko na kile cha Kambikatoto muanze kuangalia taratibu za kupata maji pamoja na umeme mapema kabisa, wananchi wamehamasika, wamechangia fedha, tukikaa muda mrefu kituo kimekamilika na hakitoi huduma itakuwa shida,” alisema Sonda.
Sambamba na hayo wataalamu toka Tamisemi wamewataka halmashauri kuongeza kasi ya ujenzi ili miradi yote ikamilike kwa wakati hasa kwenye ujenzi wa jengo la dharula katika hospitali ya wilaya.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na wataalam hao ni miradi ya sekta ya Afya ambapo walitembelea kituo cha afya Kambikatoto, Mafyeko na Ujenzi wa majengo unaoendelea katika Hospitali ya wilaya pamoja na Ujenzi wa jengo la Utawala.
Ujenzi wa jengo la Utawala halmashauri ya wilaya ya chunya
Wataalamu toka OR TAMISEMI, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Wataalamu toka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya chunya wakikagua ujenzi wa jengo la Utawala.
Ujenzi wa Jengo la Dharula katika hospitali ya wilaya
Ujenzi wa kituo cha Afya kambikatoto
Wataalamu wakikagua ujenzi wa Nyumba ya Mganga 3 in 1 Katika kituo cha afya cha Kambikatoto
Wataalamu Toka OR Tamisemi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa sambamba na wataalamu toka Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakikagua ujenzi wa jengo la OPD katika kituo cha afya Mafyeko
Ujenzi wa kituo cha afya Mafyeko
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.