Taasisi ya kuziua na kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Chunya imewafikia waganga wafadhi wa vituo vya Afya na zahanati zote zilizopo wilayani Chunya ili kutoa Elimu ya namna ambavyo wanaweza kuungana na Taasisi hiyo kuzuia na Kupambana na Rushwa jambo litakalopelekea wao kama watumishi wakawa salama lakini lengo la huduma bora kwa watanzania likatimizwa bila upendeleo.
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo leo tarehe 20/09/2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Afisa kutoka TAKUKURU wilaya ya Chunya Ndugu Gift Chihimba amewataka waganga wafawidhi kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu na miongozo wanapowahudumia wananchi wao, kwa njia hiyo watakuwa wametekeleza majukumu yao vizuri lakini wanakuwa wamemsaidia Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupeleka Huduma stahiki kwa wanannchi wa Tanzania wakiwepo wananchi wa wilaya ya Chunya
Mganga Mkuu wa wilaya ya Chunya Dkt Darison Andrew amesema kikao hicho kinapaswa kufanyika kila robo ya mwaka kikilenga kufanya tathimini kwa ujumla ya hali ya Afya na kupitia kikao hicho ndipo maeneo ya kuongeza mkazo hudhihirika na kuwekewa mikakati na mipango ya pamoja.
“Kikao hiki kinapaswa kufanyika kila robo mwaka na lengo lake ni kufanya tathimini ya utoaji wa huduma kwa ujumla na tumewaalika TAKUKURU kwa lengo la kutoa elimu kwa watumishi hawa ili wawe na ufahamu wa mambo mbalimbali ya kufanya na mambo ambayo hayapaswi kufanya wakati wakiendelea kuwahudumia wananchi wa Chunya" amesema Dkt Darison
Pamoja na mafunzo hayo waganga wafawidhi wa vituo hivyo wamepaza sauti kutoka Elimu iendelee kutolewa ili wanaume (Wakina baba) Watambue umuhimu wa wao kuongozana na wenza wao kwenda vituo vya kutolea huduma ili kupata ushauri wa kidaktari pamoja na kwa kufanya hivyo dalili za Rushwa na upendeleo zitakuwa zimekomeshwa jambo ambalo litapunguza zaidi vifo vya Mama wajawaziti na watoto
“Wanaume hawaongozani na wenza wao kwenda vituo vya kutolea huduma kama utaratibu ulivyokuwa umetangazwa hapo awali na tunapochukua hatua ili angalau kuhimiza wanaume kuongoza/kuambata na wenza kuja kwenye vituo vya kutolea huduma tunaanza kunyooshewa vidole kwamba tunakiuka Sheria na taratibu za kazi sasa mnapokpata nafasi Elimu iendelee kutolewa juu ya umuhimu wa wanaume kuongozana na wenza wao” Amesema Febi Ambangile
Kwa niaba ya waganga wafawidhi wengine Dkt Paul Saigod na Neema Mwafulilwa wamesema baadhi ya makosa yanatokana na mazingira yenyewe hivyo wamewaomba wasimamizi wa Sheria kutazama pande zote mbili wanaposimamia sheria hizo kuamua juu ya changamoto zinazokuwa zimejiokeza kwani wakati mwingine changamoto inajitokeza sio kwa makusudi.
Elimu ya Mapambano dhidi ya Rushwa ikiwafikiwa vizuri watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla itasaidia kuweka usawa na haki na upatikanaji wa huduma katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya na Tanzania kwa ujumla jambo ambalo litapelekea kila mtanzania kufurahia maisha ndani ya nchi yake.
Afisa kutoka TAKUKURU Chunya Bwana Gift Chihimba akiendelea kutoa Elimu wakati wa kikao cha Waganga wafawidhi wa vituo vya Afya na Zahanati wilayani Chunya kilichoketi kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya uliopo kwenye Jengo Jipya la utawala
Febi Ambangile (Aliyekaa na amenyoosha mkono) ambaye ni moja katia ya washiriki wa Mafunzo hayo akifafanua jambo kwa Afisa TAKUKURU wakati wa wasilisho lake
Bwana Paul Saigod (Aliye simama akionekana akizungumza kwa vitendo) ni moja ya washiriki wa kikao hicho na hapo alikuwa akifafanua jambo wakati wa wasilisho kutoka kwa afisa TAKUKURU wilaya ya Chunya
Mfamasia wa wilaya ya Chunya Dkt Edward Tengulaga akiendelea na wasilisho lake wakati wa Kikao na Waganga wafawidhi wa vituo vya Afya na Zahanati zilizoko wilayani Chunya kilichoketi Mapema leo ili kufanya tathimini ya utoaji wa Huduma kwa Ujumla wake
Waganga wafawidhi wa vituo vya Afya na Zahanati wilayani Chunya wakiwa wanafuatilia Mafunzo kutoka kwa Afisa TAKUKURU pamoja na Mada nyingine zilizowasiliwashwa mapema leo wakati wa kikao cha Tathimini wa utoaji wa huduma
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.