Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga amewataka watendaji wa kata na vijiji pamoja na Jamii kwa ujumla kushiriki ipasavyo katika suala la Lishe kwa Familia zao na Jamii kwa ujumla kwani kwa kufanya hivyo ni kuisaidia Jamii ya sasa na ya baadaye kiafya, kiuchumi na Kijamii jambo ambalo litahakikisha ustawi wa Jamii ya wanachunya na Taifa kwa Ujumla
Akiongoza kikao cha Lishe kwa robo ya tatu ya mwaka 2023/2024 kilichoketi leo tarehe 2/5/2024 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ulipo jengo jipya la utawala amewataka watendaji wa kata na Vijiji kutokuwaachia wahudumu wa Afya ngazi za kata na vijiji kusimamia suala la Lishe bali washirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha Jamii inatambua na inazingatia suala la Lishe kama mikataba inavyoelekeza.
“Kila mtendaji anapaswa kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za lishe, msiwaachie wahudumu wa Afya ngazi za kata na vijiji wasimie suala la Lishe. Tunaondoka hapa tukiwa na kauli moja wanafunzi wote wa madarasa ya awali bila kuacha wanafunzi wa madarasa mengine kuanza kupata Chakula wanapokuwepo Shule. Lakini pamoja na kuwepo mikata tuliyosaini inayotutaka tusimamie suala la Lishe, Watendaji wote waandikiwe Barua ya kuwataka kusimamia vizuri suala la Lishe ili akitokea mtu analega basi tumchukulie hatua stahiki” amesema Mhe Batenga
Akichangia mjadala wa uongezaji wa virutubisho kwenye unga Afisa biashara wa wilaya ya Chunya ndugu Rodrick Mwakisole amesema kama Elimu ya namna ya kuongeza virutubisho ikiwafika vema waanchunya watapata fursa kubwa zaidi ya kibiashara na hatimaye kuongeza vipato vyao na baadaye kuongeza pato la Halmashauri na Taifa kwa Ujumla.
“Suala la Lishe pamoja na kuimarisha Afya za watoto wetu na jamii kwa ujumla lakini katika mchakato wa kuongeza virutubisho kuna fursa kwa wananchi kiuchumi kwani kupitia kufunga vifaa vya kuongeza virutubisho vitaongeza idadi ya watu kuja kusaga katika mashine hizo na baadaye fursa nyingine zitaendelea kufunguka hivyo ni vema wananchi wakaelimishwa juu ya suala hilo”
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dkt Darison Andrew pamoja na kushukuru usimamizi mzuri wa mwenyekiti katika suala la Lishe, ameendelea kuwahimiza watendaji wa kata na vijiji na hata wanajamii kuongeza juhudi ya kuzingatia lishe kwa jamii yao kwani athari za ukosefu wa lishe ni kubwa na ngumu kurudi katika hali ya kawaida ikitokea athari hizo zikijitokeza katika jamii zetu.
“Tukiwekeza kwenye lishe Itasaidia kuwa na kizazi sahihi na chenye uwezo mzuri wa kufikiri. Hivyo watendaji wa kata na vijiji kwa nafasi zenu endeleeni kutoa Elimu hii kwa wanajamii na tukifanya hivyo tutakuwa tumeoka familia zetu na hata Taifa kwa ujumla, Gharama za udumavu ni kubwa sana hivyo tupambane pamoja kuondokana na udumavu huo” Amesema Dkt. Andrew
Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Rehema Hiluka amemshukuru Mkuu wa wilaya ya Chunya ambaye ndiye mwenyekiti wa Kikao cha Lishe kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa Mbele kuhakikisha suala la Lishe linazingatiwa na viongozi pamoja na wananchi huku akihimiza ushirikiano kati ya viongozi na wananchi katika kuhakikisha suala la lishe linazingatiwa katika maeneo yao
Kikao cha lishe kwa robo ya tatu 2023/2024 kimehudhuriwa na watendaji wa Kata na vijini Halmashauri ya wilaya ya Chunya pamoja na wakuu wa idara na vitengo wanaotekeleza Afua za Lishe na kilihusisha upimaji wa uzito, urefu pamoja na Kisukari kwa hiari ikiwa ni kuwajali wajumbe wa kikao pamoja na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya.
Afisa Biashara wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Rodrick Mwakisole akiwasilisha jambo kwenye kikao cha Lishe robo ya tatu 2023/2024 kilichoketi leo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Jengo Jipya la Utawala
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Dkt Darison Andrew akisisitiza Jambo wakati wa kikao cha Lishe kwa Robo ya Tatu kilichoketi tarehe 2/5/2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Jengo Jipya la utawala)
Afisa Lishe wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Rehema Hiluka akizungumza Jambo wakati wa kikao cha Lishe kwa Robo ya tatu ya mwaka 2023/2024
Mtendaji wa kata ya Kasanga Ndugu Lwitiko Mwalugaja akifafanua Jambo wakati wa kikao
Afisa Lishe wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Rehema Hiluka akiwasilisha taarifa ya Umuhimu wa kuongeza virutubisho kwenye unga wakati wa kikao cha Lishe cha Robo ya Tatu mwaka 2023/2024
Afisa Lishe Ndugu Saimon Mayala anayesoma kwenye Mzani) akitazama urefu wa Mtendaji wa kata ya Lualaje tayari kulinganisha na urefu wake wakati wa zoezi la kupima urefu, uzito na kisukari leo wakati wa kikao cha Lishe kwa robo ya tatu mwaka 2023/2024
Wahudumu wa Afya wakiendelea kutoa huduma ya vipimo vya urefu, uzito, Kisukari na Presha wakati wa kikao cha Robo ya tatu ya mwaka 2023/2024 kilichoketi leo tarehe 2/5/2024
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.