Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya wilaya ya Chunya imewataka viongozi wa serikali na wananchi kusimamia pesa za serikali ipasavyo ili kufikia lengo la serikali la kuleta fedha kutekeleza miradi katika meeneo mbalimbali ya wilaya ya Chunya kufikiwa
Kauli hiyo imetolewa leo terehe 04/10/20234 na kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kupitia mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Bosco S. Mwanginde wakati alipoiongoza kamati hiyo kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambapo kupitia ziara hiyo kamati ilifanikiwa kukagua miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni mbili
“Simamieni pesa hizi kama zenu kwani kwakufanya hivyo pesa nyingine zinazobaki zitatumika kuanza kujenga mradi mwingine eneo lingine lakini mnanunua dawati shilingi elfu hamsini (50,000) eneo hili la Mpembe wakati mnayo miti mingi kuliko maeneo mengine tuliyopita! haiwezekani kabisa”
Aidha Mwenyekiti wa kamati hiyo aliongeza kusema “ Wataalamu hamtusaidii kabisa yaani mnaacha mafundi wanaharibu thamani zilizonunuliwa kwa fedha za serikali, wanaharibu saruji, malumalu yaani hamsimamii miradi ya maendeleo ipasavyo jambo linalopelekea kukwama kwa mradi au kutokamilika kwa fedha zilizotengwa” aliongeza Mhe Mwanginde
Katika kukamilisha ziara hiyo kamati ilitembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Mapogolo iliyopo kata ya Chokaa ambapo ilipongeza usimamizi mzuri wa mradi huo kwani umekamilika kwa wakati na samani zilizowekwa ndani ya madarasa hayo zimefuata maelekezo ya serikali
Diwani wa kata ya Chokaa Mhe Samwel Komba kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo amewashukuru kamati kwa ujumla wake kwanza kuwapatia fedha za kutekeleza mradi huo lakini pia amesema bado kata ya Chokaa inauhitaji sana hivyo amewaomba wakiona inafaa waendelee kuwapatia fedha ili waendelee kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kiwango ambacho serikali inaagiza
Ziara ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikihusisha wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya ilianza tarehe 2/10/2023 na kutamatika tarehe 4/10/2023 ambapo miradi mbalimbali imekaguliwa huku maoni na maagizo mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa kamati hiyo yakitolewa ili kuboresha zaidi ujenzi wa miradi hiyo.
Vyumba viwili na ofisi vilivyojengwa katika shule ya msingi Mpembe na wanaoonekana ni wajumbe na wataalamu wa kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wakiendelea na ukaguzi wa mradi ukilinganishwa na fedha zilizopelekwa kutekeleza mradi huo
Diwani wa kata ya Kasanga na Mjumbe wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Mhe. Mh. Benson B. Msomba akichangia jambo wakati wa ziara ya kamati hiyo walipokuwa wanakagua ujenzi wa matundu ya Vyoo shule ya Msingi Mpembe
Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Mhe Bosco S Mwanginde akitoa maagizo ya Kufukiwa Shimo lililokuwa limechimbwa kwaajili ya kuhifadhi maji wakati wa ujenzi wa madarasa kwani linahatarisha usalama wa wanafunzi wawapo shuleni
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.