• Malalamiko |
    • wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
Chunya District Council
Chunya District Council

jamhuri ya muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za mikoa na serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Chunya

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • muundo wa Taasisi
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Mipaka ya Kiutawala
    • Idara
      • Utumishim na Utawala
      • Mipango,ufuatiliaji na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Tehama
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha, Utawala, Mipango
      • Afya, Elimu, Maji
      • Maadili
      • Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao
      • Mwenyekiti kuonana na Wananchi
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ambayo haijakamilika
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu wa kufuata
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu za maombi
  • kituo cha habari
    • taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba mbali mbali
    • Maktaba ya picha
    • matukio mbali mbali
    • Habari

SERIKALI WILAYANI CHUNYA IKO TAYARI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA CRDB.

Imewekwa: November 6th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaj Batenga ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano muda wote utakapo hitajika kwa benki ya CRDB kwani benki hiyo imekuwa  mdau muhimu  wa maendeleo kwani  wameendelea kushirikiana  katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 6 Novemba 2024 ofisini kwake  alipotembelewa na wadau kutoka benki ya CRDB kanda ya nyanda za juu  kwaajili ya mazungumzo ili kuendelea kukuza na kuboresha huduma zao.

Aidha Mhe Batenga  ametoa pongezi kwa benki ya CRDB kwa kuwa na huduma ya kibenki  inayotembea  (bank mobile service) hususani kwa maeneo ambayo hakuna matawi ya benki hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wanaowahudumia katika maeneo  yao wanayoishi  au maeneo wanayofanyia kazi.

“Niwapongeze kwa kuwa na  huduma inayotembea (mobile service)  ambayo inasaidia sana kwa wakulima wetu huhssani kwa maeneo kama lupa  na  wakati mwingine ni vyema mkafanya utafiti wenu kuona uwezekano wa kufungua tawi Lupa ili kuwapunguzia adha wateja wenu kusafiri umbali mrefu kufwata huduma lakini pia kwa usalama wa fedha za wateja wenu”amesema Mhe.Batenga

Naye Meneja wa Biashara benki ya CRDB  kanda ya ya nyanda za juu  Bi Domina Mwita amesema kuwa lengo la ziara yao  ni kutoa shukrani  kwa Uongozi wa Wilaya ya Chunya kwa ushirikiano ambao wameendelea kuutoa kwao kamawadau wa benki hiyo lakini pia kufahamiana na kuona namna ya kuongeza wigo Zaidi wa kuwahudumia wanachunya katika Nyanja tofauti tofauti.

Bi Domina pia amekiri kupokea maoni yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya na kuahidi kuyafanyika kazi ili kuendelea kuboresha Zaidi huduma zao  ikiwa ni pamoja na kuona namna ya kuwasaidia  mikopo wachimbaji  wadogo ili kukuza mitaji yao lakini pia kuendelea kutoa elimu za kifedha kwa wadau wao ili kukuza uelewa .

Wafanyakazi wa benki ya CRDB wametembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya  kukutana na viongozi wengine na  wadau mbalimbali   wa Chunya na kufanya nao mazungumzo ili kuboresha na kukuza huduma zao pamoja na  kuzichukua changamoto mbalimbali zinazowakumba  wateja wao ili kufanya maboresho .

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaj Batenga akizungumza na wadau kutoka benki ya CRDB kanda ya nyanda za juu  walipomtembelea ofisini kwake kuona namna kukuza  na kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Chunya.

Meneja wa biashara benki ya CRDB kanda ya nyanda za juu Bi Domina Mwita akielezea namna ambavyo wamejipanga kuboresha na kukuza huduma zao kwa wananchi wa Wilaya ya Chunya wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ofisini kwake.

Wafanya kazi wa Benki ya CRDB wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya wakati walipoketi ofisini kwake kwaajili ya mazungumzo juu ya huduma zao zinazotolewa   na namna ya kuendelea kukuza huduma zao.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Mbaraka Alhaj Batenga wa pili kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB kanda ya nyanda za juu  baada ya kumaliza mazungumzo yao .




Matangazo

  • ORODHA YA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA JIMBO LA LUPA December 21, 2024
  • Tangazo la Kuitwa kwenye usaili Kazi za MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 July 17, 2022
  • Orodha ya walioitwa kwenye usaili Maombi ya kazi za sensa_Chunya_2022 July 17, 2022
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI 2022, HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA July 22, 2022
  • Zaidi

Habari Mpya

  • ZINGATIENI WELEDI NA UFANISI KAMA MLIVYOAMINIWA

    April 29, 2025
  • MAAFISA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI KUNOLEWA ZAIDI JUU YA AFYA YA AKILI.

    April 16, 2025
  • DC CHUNYA NA SONGWE WAPELEKA OMBI MOJA KWA WAZIRI.

    April 04, 2025
  • TARAFA YA KIPEMBAWE CHUNYA YAJIDHATITI KUWATUMIKIA WANANCHI.

    March 21, 2025
  • Zaidi

Video

BILIONI 2.2 BAJETI YA TARURA WILAYA YA CHUNYA, SERIKALI TUNASHUKURU
video zaidi

Kiunganishi cha haraka

  • HATUA ZA KUANZISHA BIASHARA
  • MIONGOZO MBALIMBALI
  • FOMU ZA HUDUMA MBALIMBALI

Tovuti Nyingine Tunazohusiana

  • OR-TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI
  • majukumu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na Sheria ya Serikali Mtandao kwa ujumla
  • MKOA WA MBEYA
  • WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
  • WAKALA WA SERIKALI MTANDAO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

wasiliana nasi

    Itigi Road

    sanduku la posta: P.O box 73 Chunya

    simu ya mezani: 025 2520121

    simu ya mkononi: 025 2520121

    Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera binafsi
    • kanusho
    • MMM
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.