Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga amesema Serikali wilaya ya Chunya itaendelea kupokea maelekezo ya Chama na kuyatekeleza pamoja na kuhakikisha yale yaliyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi yanatekelezwa kwa asilimia mia moja ili kuondoa maswali kwa wananchi wa Chunya kuhoji uhitaji au ubovu wa miundombinu yoyote ile ya utoaji wa huduma.
Ametoa kauli hiyo tarehe 30/5/2024 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Igundu kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Igundu wakati wa Hafla ya kukabidhiwa mradi wa Maji uliotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia RUWASA, Shirika na Catholic Relief Services (CRS) pamoja na wananchi wa Igundu
“Sisi kama Serikali tunaahidi kuendelea kupokea maelekezo ya Chama na kuyatekeleza ili kuondoa Maswali kutoka kwa wananchi kuhusu Serikali yao, Wananchi waendelee kuiamini Serikali yao kwani ni sikivu na yenye kuwajali wananchi wake” Alisema Mhe Batenga
Diwani wa kata ya Sangambi Mhe Junjuu Muhewa kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Igundu na Kata ya Sangambi kwa ujumla amewashukuru Shirika na Catholic Relief Services (CRS) pamoja na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupelekewa fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa maji uliokabidhiwa kwa wananchi wa Igundu baada ya kukamilika kwa asilimia mia moja
“Nimehemewa na furaha kwasababu ya furaha, Naomba nitoes Shukrani zangu kwa Shirika hili la CRS linalofanya kazi kwa karibu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan. Pamoja na Mradi huu wa Maji tunaokabidhiwa leo kata yangu ya Sangambi imepokea fedha zaidi ya Bilioni Mbili kutekeleza miradi mbalimbali hivyo naomba nipelekee salamu zangu na za wananchi hawa wa Igundu na wananchi wa kata ya Sangambi kwa Mhe Rais Samia kwamba wanasangambi tunamshukuru sana” Amesema Mhe Junjulu
Meneja wa RUWASA wilaya ya Chunya Mhandisi Olineno Sanga amesema utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye sekta ya Maji wilaya ya Chunya imefikia asilimia themanini na tano (85%) huku akisema mipango yao ifikapo 2025 kata ya Sangambi itafikia asilimia mia moja katika upatikanaji wa Maji safi na salama kwa matumizi ya Binadamu
“Kwa maana ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tumeshafikia azma ya Serikali kwa maana ya asilimia themanini na tano (85%) lakini pia tumekuwa na mipango mbalimbali tumebakiza kijiji kimoja cha Shoga lakini pia kitongoji kimoja cha Dendeluka, Rais ameshatoa fedha kwaajili ya upatikanaji wa Maji kwenye maeneo hayo na ni matumaini yetu ifikapo 2025 tutafikia asilimia mia moja upatikanaji wa maji katika kata ya Sangambi” Amesema Mhandisi Sanga
Mkuu wa ofisi ya CRS Mkoa wa Mbeya Bi Marilyn Chottah amesema, Mradi huo umegharimu shilingi milioni mia nne thelasini na nne huku asilimia Zaidi ya themani ya fedha hizo zikitolewa na shirika la CRS na mradi unalenga kuwahudumia wananchi 4883 wa Kijiji cha Igundu huku Taasisi za Serikali kama vile Zahanati ya Igundu na Shule ya Msingi ya Igundu zikinufaika moja kwa moja na mradi huo kwa kujengewe miundombinu mbalimbali ya maji ambayo imeunganishwa moja kwa moja na maji hayo
“Mradi huu umegharibu shilingi milioni mia nne thelasini na nne elfu mia mbili sabini na tano na laki tatu na hamsini na sita elfu (434,275,356,000/=) huku ashilingi miliomni ia tatu sabini na tano ambazo ni sawa na silimia 86.5% ya fedha zote za mradi zikitolewa na shirika na Catholic Relief Services CRS na Lengo na Mradi ni kuwahudumia wananchi wa Igundu ili waepukane na changamoto ya maji” Amesema Bi Chottah
Shirika na Catholic Relief Services (CRS) linatekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya huku Mradi wa Ifumbo umeshakamilika na unatumika, Mradi wa Igundu kata ya Sangambi umekamilika na umekabidhiwa Jana tarehe 30/5/2024 na Mradi mwingine unatekelezwa kata ya Kasanga kijiji cha Soweto umefikia asilimia karibu Themanini (80%) na Lengo kubwa ya CRS ni kuhakikisha linashirikiana na Serikali kutatua changamoto za wananchi wa wilaya ya Chunya zinatatuliwa kwa wakati.
Mhandisi wa RUWASA Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhandisi Olineno Sanga akifafanua Jambo wakati Mkuu wa wilaya ya Chunya akikagua miundombinu ya mradi wa Maji wa Igundu Kabla ya kuukabidhi kwa wananchi baada ya kukamilika kwa asilimia mia moja tayari kwa matumizi ya Mradi huo
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuupokea mradi wa Maji uliotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali, CRS pamoja na wananchi wenyewe kwenye Kata ya Sangambi kwenye kijiji cha Igundu
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.