Usiku wa kuamkia tarehe 23/8. Ni siku ya Sensa na itabaki kuwa tarehe rejea ya siku ya sensa. Kuhesabu Watu kutaendelea kwa takribani siku 6 hadi saba kwa kuzingatia tarehe rejea. ieleweke kuwa sensa haiwezi kukamilika kwa siku moja kwa nchi nzima. Hivyo hata ukipumzika inawezekana siku hiyo Kaya yako isifikiwe hivyo hakuna mantiki ya kupumzika kwa wale wanaofanya vibarua au Kazi za kila siku. Unachotakiwa kufanya ni kuorodhesha na kuandika kwenye karatasi watu wote watakaolala Kwenye kaya yako usiku wa kuamkia siku hiyo
Taarifa muhimu ni pamoja na:
1. Jina kamili (matatu)
2. Jinsia (me/ke)
3. Umri
4.Hali ya ndoa
5. Namba ya simu
6. Namba Nida
7. Taarifa za Elimu
8. Taarifa za hali afya
9. Umiliki wa Ardhi, Majengo, vifaa/rasilimali
10. Taarifa ya Shughuli za Kiuchumi
11. Mengineyo (uraia)
Pamoja na kuacha Taarifa hizo karani atakupigia simu kuhakiki Taarifa ulizoacha tafadhari toa ushirikiano.
NB:Kwenye namba ya NIDA / vitambulisho vingine vya kitaifa kama Bima ya Afya, leseni ya Udereva, Hati ya Kusafiria kama mwanakaya au wanakaya wanavyuo
Mimi niko tayari kuhesabiwa . WEWE je?
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.