Kambi ya maandalizi iliyodumu kwa wiki Mbili hapo Shule ya Sekondari Chokaa ya timu inayotaraji kuiwakilisha Chunya kwenye michezo ya SHIMISEMITA mwezi August imejipima nguvu kwa mchezo wa kirafiki ambapo leo 19/07/2025 imeichalaza vibaya timu ya Halmashauri ya wilaya ya Rungwe katika michezo mbali, Michezo iliyochezwa kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Isenyela iliyopo kata ya Mbugani wilayani Chunya
- Mpira wa Miguu Me Chunya 5: Rungwe 2
-Handball (Me) Chunya 7: Rungwe 2,
-Handball (Ke) Chunya Dc 5: Rungwe 2
-Mpira wa Pete Maarufu Netball (Ke) Chunya14: Rungwe 19
Kiongozi wa timu ya watumishi Chunya Bwana Ridhiwan Mshigati anasema timu imeanza vizuri na ni matarajio ya uongozi wa wilaya ya Chunya kwamba timu itafanya vizuri Zaidi ukilinganisha na ushindi wa mwaka jana ambapo timu ya Chunya ilikuwa bingwa kuvuta kamba huku wakichua nafasi ya tatu kurusha tufe
Endelea kutufutilia kwenye mitandao yetu ili upate matokeo yote ya maandalizi ya timu hiyo na hatimaye kurudi na ubingwa, Chunya hainajawai kuwa na jambo dogo
Timu zote mbili zikiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuwavaa Timu ya Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mapema leo
Timu ya Mpira wa Miguu ikiwa katika Picha ya Pamoja kabla ya Mchezo wao wa Kirafika Mapema leo katika uwanja wa Shule ya Sekondari Isenyela Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.