Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Zuberi Homera amemwagiza Mkuu wa polisi wilaya ya Chunya (OCD) kuhakikisha anawakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria watu wote wanaotuhumiwa kuiba mahindi ya wananchi katika kata ya Lupa pamoja na vibaka wote wanaotajwa kusumbua wananchi maeneo mbalimbali wilayani Chunya
Mhe Homera ametoa maagizo hayo alipokuwa anazungumza na wananchi katika mkutano wa Hadhara uliofanyika Juni 14, 2023 katika viwanja vya ofisi ya serikali ya kijiji cha Itewe kilichopo kata ya Itewe wilyani Chunya ikiwa ni kuhitimisha ziara yake aliyoifanya ya kutembelea ujenzi wa Daharia (Bweni) ya wasichana shule ya sekondari Itewe inayojengwa kwa kushirikiana na wananchi, ofisi ya mkurugenzi, wadau, ofisi ya mbunge pamoja na Mfadhiri COCOA FOR SCHOOLS ambaye atakamilisha jengo hilo pamoja na kuweka vifaa vya ndani ambavyo ni vitanda na magodoro
“Mkuu wa polisi nakuagiza ndani ya siku saba (7) wahalifu wote walioiba mahindi wawe wamekamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria’’ alisema mhe. Homera.
Aidha Mhe. Homera alimwagiza mkandarasi aliyepewa kujenga mradi wa maji wilayani Chunya utakaogharimu kiasi cha Shilingi bilioni kumi na moja (11) kuripoti ofisini kwake ndani ya siku saba (7) ili kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wahandisi wa maji walioko ofisi ya Mkuu wa Mkoa jambo litakalopelekea kupata chanzo sahihi cha Maji wilayani Chunya ili kuondoka na adha ya maji kwa wananchi wa Chunya Mjini
“Natoa siku saba Mkandarasi huyu awe ameripoti ofisini kwangu, maana haiwezekana mkandarasi anakuja kutekeleza mradi mkoani kwetu alafu hajariporiti ofisini kwetu, na asiporipoti ofisi kwangu nitamwandikia Mhe Rais Barua ya kutokuwa na Imani na Mkandarasi huyo hivyo hawezi kutekeleza” alisema Mhe. Homera
Diwani mwenyeji wa kata ya itewe Mhe. Alex Kinyamagoha aliwashukuru na kuwapongeza viongozi na wananchi kwa ujenzi wa daharia (Bwenia) hiyo na kuwaomba wananchi kuendelea kuwa na utayari wa kuchangia kunapo kuwa na miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa chunya kwa sasa inapendeza kutokana na kuwepo kwa taa za barabarani
Baadhi ya wananchi walitoa kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja na changamoto ya maji wa kilalamikia mabomba kutokutoa maji kwa muda mrefu, wazee wa mila kusahaurika,kukosekana kwa maji na umeme katika soka la kijiji cha itewe lakini pia uwepo wa wezi ambao wamekuwa wakiwaiibia watu wanapokuwa katika shughuli zao zakila siku.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.