Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera amesema serikali inataka wawekezaji wengi waendelee kuwekeza kwenye sekta ya madini ili kuendelea kuleta tija katika uzalishaji wa madini huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwajali kwakuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwao ikiwa ni pamoja na kusogeza masoko ya dhahabu, kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya kuchimbia dhahabu na hata kemikali zinazotumika katika zoezi zima la Uchenjuaji wa dhahabu
Mhe: Homera amewataka viongozi wa serikali pamoja na jeshi la polisi kuhakikisha wawekezaji waliowekeza katika uchimbaji dhahabu wanakuwa salama wakati wote ili waweze kutoa mchango wao kwa serikali kama wanavyoendelea kutoa sasa, kwa kulipa kodi kwa wakati na kutoa ajira mbalimbali kwa wananchi na hatimaye kuleta maendeleo kwa Taifa.
Mkuu wa Mkoa yuko katika ziara ya siku mbili kutembelea sekta ya madini katika mkoa wa kimadini chunya ambapo ameshatembelea ghala la RM KYANDO COMPANY LTD ambapo amekagua mitambo na kemikali mbalimbali za kuchenjulia dhahabu, pia ametembelea maabara inayohusika na shughuli mbalimbali za upimaji wa sampuli za madini ya RM KYANDO COMPANY LTD, ametembelea Mine labs assay Geochemical analysis laboratory, Giant Machine and equipments na maeneo mengine
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewataka wananchini kutumia maabara za kisasa zilizopo katika mkoa wa madini chunya kwani zinasaidia sana katika kuchimba kwakujua eneo husika lina kiasi gani cha madini na sio kuchimba kienyeji, kwanza kuna uharibifu mkubwa wa mazingira lakini pia unaweza kutumia nguvu kubwa kuchimba eneo ambalo halina madini
“Madini hayapimwi kwa mganga wa kienyeji, bali kwa mitambo hii ya kisasa kabisa, hivyo wananchi njooni mpime sampuli za madini eneo unalotaka kuchimba na Nyinyi wenye mitambo endeleeni kuwa wabunifu zaidi wa teknolojia ya uchimbaji madini ili muweze kuwasiaidia wananchi”
Afisa madini Mkaazi wa Mkoa wa Chunya Eng. Nyansiri Sabai akizungumza mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya amesema kwasasa kemikali zote zinazotumika kuchenjulia dhahabu zinapatikana chunya jambo ambalo limewarahisishia wachimbaji kutokuhangaika kuzitafuta na ameongeza kuwa ghara lingine linalojengwa na Giant Machine and Equipments litaendelea kuleta suluhu na ahueni ya bei ya kemikali kwa wachimbaji.
“Kukamilika kwa ujenzi wa ghala hili linalojengwa na Giant Machine equipments litasaidia sana kupunguza bei ya gharama ya kemikali ikiwezekana hata chini ya bei elekezi ya serikali laki sita (600,000)” amesema Eng. Nyansiri
Awali akizungumza mbela ya Mkuu wa Mkoa Aidan Msigwa (Mdimi) ameeleza changamoto mbalimbali ambayo yeye pamoja na wachimbaji wengine wanapitia huku akipeleka ombi kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na serikali kwa ujumla wake kusaidia kuleta suluhu ili waendelee kuzalisha kwa tija na kuendelea kulipa kodi kwa mujibu wa sheria
Baadhi ya chnagamoto alizoeleza msigwa ni pamoja na taasisi za fedha kushindwa kuwaamini kuwapa kiasi cha fedha wanachohitaji ili kuendesha shughuli zao jambo linalofanya waingie kwenye taasisi zenye riba kubwa jambo ambalo linarudisha nyumba mipango yao na baadaye kushindwa hata kulipa kodi kwa wakati
Changamoto nyingine ni pamoja na bei ya mafuta (Disel) imekuwa kubwa sana kupelekea uendeshaji wa shughuli za uchimbaji kuwa ngumu, kemikali za kuchenjulia dhahabu pia ilikuwa gharama kubwa jambo linaloleta changamoto katika uzalishaji
Pamoja na mambo mengine mengi yaliyofanyika katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa amewashukuru wadau wote waliowekeza kwenye sekta ya madini kwani juhudi zao zimefanya mkoa wa kimadini chunya kuwa nafasi ya pili katika uzalishaji wa madini Tanzania ikitanguliwa na Geita na ameawataka kuendela kuongeza kasi
Katika ziara hiyo ambayo inataraji kuendelea tena Kesho tarehe 9/2/2023 Mkuu wa Mkoa ameendelea kuwaalika kwenye maonesho makubwa ya madini yanayotaraji kufanyika katika mkoa wa kimadini Chunya ambapo mambo mbalimbali yatajadiliwa huku akiwataka wadau wa madini kuhakikisha wanashiriki maoneshon hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mine labs Geochemical Analyisis Labaratory Eng. Simon Shinshi (Mwenye kofia) akitoa maelezo kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera wakati wa ziara ya kutembelea sekta ya madini katika mkoa wa kimadini chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.