Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe, Juma Zuberi Homera amesema mkoa wa kimadini Chunya unafanya vizuri sana katika sekta ya madini jambo linalopelekea uzalishaji wa madini kuongezeka kutoka kilograma 20 mpka kufikia kilogramu 330 kwa mwezi ambapo zaidi ya Bilioni thelasini hupatikana kupitia sekta ya madini
Homera amesema hayo Mapema jana wakati akifunga maonesho ya kwanza ya Teknolojia ya Madini yalitofanyika kuanzia tarehe 14/03/2023 katika viwanja vya Chunya kati vilivyopo halmashauri ya wilaya ya Chunya ambayo hutambulika kama mkoa wa kimadini Chunya
“Kwakweli Chunya mnafanya vizuri sana katika sekta ya madini kuanzia wachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogo hakika kwakweli tunastahili kuwapongeza sana sana wanachunya wote kwa kazi kubwa mnayoifanya”
Homera amesema maelekezo aliyoyatoa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kulegeza mashariti katika sekta ya uchimbaji ndiyo yanayopelekea kuwa na wawekezaji wengi wilayani chunya Huku wawekezaji wazawa kuongezeka katika sekta ya Madini
“Tumeshuhudia wawekezaji wengine wamewekeza kwenye sekta ya madini hapa wilayani Chunya, tumejionea makampuni makubwa kama vile Ramani Investment, kina Achimwene, Kindai Investment, Sunshine, Msigwa na mengine mengi, Yote haya ni kutokana na maelekezo aliyoyatoa Mhe. Rais ya kulegeza mashariti ya kuingiza vifaa vya uchimbaji hivyo ni lazima tumpongeze sana Mweshimiwa Rais kwa kuamua kuwekeza kwenye sekta ya Madini”
Kwakukumbuka kifo cha Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. Dkt John Joseph Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewaongoza wananchi waliojitokeza katika maonesho hayo kutulia kwa dakika moja ikiwa ni ishara ya kumkumbuka, kuenzi na kumwombea kheri apumzike kwa amani huko aliko
Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Katibu tawala wa Mkoa wa Mbeya ndugu Rodrick Mpogolo amsema sekta ya madini ina Mchango mkubwa kwa Taifa na kwa jamii kuanzia ngazi ya familia na kaya moja moja hivyo kupitia maonesho haya ni imani yetu wachimbaji wamepata elimu, fursa mbalimbali zimefunuliwa na mambo mengine
Aidha katibu tawala huyo amesema maonesho haya yalianza rasmi tarehe 14 mwezi machi na kutamatika tarehe 18 machi hivyo wafanyabiashara na wadau wote wa madini wametakiwa kuendelea kutumia fursa hiyo ya kukutana na wafanya baishara mbalimbali na wadau wa madini kutoka Chunya na nje ya Chunya ili kuendelea kukuza vipato vyao
Awali akitoa salamu za wachimbaji kwa Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa wachimbaji katika mkoa wa imadini Chunya Ndugu Leonard Manyesha amewasilisha kilio cha wachimbaji kwa Mkuu wa Mkoa huo ambazo ni pamoja na Tozo kuto Mamala ya mapata Tanzania, Taasisi za kifedha kutowaamini wachimbaji na kuwakopesha ili waendeleze shughuli zao za kiuchimbaji
“Sisi wachimbaji tunaimani kubwa sana kwa serikali hii hivyo kupitia Maonesho haya tunaamini changamoto zetu zinaenda kutatuliwa mfano Tozo za TRA, tunaamini uchimbaji katika Mkoa huu utaendela kukua zaidi, Pia tunaomba taasisis za kifedha kuwakopesha wachimbaji. Na tuna amini maonesho haya yataendelea kuwepo kila mwaka ili wachimbaji waendelee kujifunza fursa mbalimbali zilizopo katika madini”
Maonesho ya Teknolojia ya Madini yamefanyika kwa mara ya kwanza katika Mkoa wa Kimadini Chunya kuanzia tarehe 14 march na kutaraji kutamatika tarehe 18 machi 2023 ambapo wadau mbalimbali wa sekta ya madini wamekutana kubadilishana uzoefu katika sekta hiyo na kauli mbiu ya maonesho hayo ilikuwa ni “Uongezaji wa thamani ya madini kwa maendeleo ya taifa”
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.