Wakulima wa zao la Tumbaku Mkoa wa kitumbaku Chunya waaswa kutotorosha Tumbaku kwani watakaobainika kutorosha au kuweka uchafu kwenye Tumbaku watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani sambamba na kutaifishiwa Tumbaku yao.
Kauli hiyo imetolewa Mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera kwenye uzinduzi wa soko la tumbaku uliofanyika katika ghala la AMCOS ya kijiji cha Kalangali kata ya mtanila wilayani Chunya
“Niwaombe vyombo vya ulinzi na usalama mtu anayeweka mawe kwenye Tumbaku, Mnyimeni dhamana, ni uhujumu uchumi. Hatuwezi tukaharibi taswira ya mkoa wa Mbeya na Songwe kwa kuweka mawe kwenye Tumbaku, Mkimkamata huyo mtu hakuna kumuonea huruma” Mhe Homera
Homera pia amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Chunya kutaifisha Tumbaku itakayokamatwa ikitoroshwa kutoka Chama kimoja kwenda Chama Kingine au ikitoroshwa kwenda nje ya Mkoa wa Kitumbaku Chunya jambo ambalo halikubaliki kulingana na miongozo ya kilimo cha zao la Tumbaku
“Anaye torosha Tumbaku kupeleka kwenye chama kingine mkimkamata Mhe. Mkuu wa wilaya beba hiyo tumbaku inarudi kwenye chama alichotoka itaifishwe asilimia 70 wapate wenyewe kwenye chama na asilimia 30 iende Halmashauri” Homera
Homera amewataka wananchi kuhakikisha hawachanganyi tumbaku na vitu vingine kwani kufanya hivyo ni kujiharibia wao wenyewe, kitu ambacho kitapelekea makampuni kuondoka na kuacha kununua Tumbaku huku akiwaonya viongozi wa Vyama vya Msingi kuhakikisha Tumbaku haichanganywi na mawe kwani chama kitakachobainika kuruhusu wakulima wake Kuchanganya mawe chama hichi kitafutuiwa usajili.
“Niwaambie ni chama ambacho kitapokea Tumbaku ya namna hiyo hicho chama tutakifuta, wanachama mtaenda kwenye vyama vingine, lazima na chama cha msingi muwe makini, huwezi mkaruhusu tumbaku iwekwe mawe” alisema Mhe. Homera
Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbarak Alhaji Batenga ametoa rai kwa wakulima wa zao la Tumbaku kuendelea kuhifadhi mazingira na kuhakikisha wanapanda miti ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaoambatana na kilimo cha zao la Tumbaku
“Zao hili la Tumbaku tumekuwa tukiendeleza kama takwimu ambavyo zinasema, yapo mambo ya msingi wakati tunazalisha na yenyewe tuyazingatie, Mhe Mkuu wa mkoa nimejipa jukumu la kusimamia swala la mazingira ili lisilete changamoto katika biashara yetu hii ya dhahabu ya kijani” Mhe Batenga
Hafla ya ufunguzi wa Msimu wa masoko ya Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Chunya imefanyika mwishoni mwa juma (Mei 17, 2024) katika ghala la AMCOS ya kijiji cha Kalangali kata ya mtanila wilayani Chunya ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alikuwa Mgeni rasmi katika Hafla hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera aliyevaa miwana, kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe. Mbarak Batenga na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika CHUTCU Mhe. Sebastian Masika, akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Msimu wa soko la Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Chunya Hafla iliyofanyika katika ghala la AMCOS ya kijiji cha Kalangali kata ya mtanila
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma zuberi Homera akiandika aina ya Daraja katika belo la Mkulima wakati wa Ufunguzi wa Msimu wa Masoko ya Tumbaku
Muonekano wa mitumba ya tumbaku katika Ghala la AMCOS ya kalangali
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.