Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amesema lengo la kutembelea Maonesho ya nanenane ni pamoja na kujionea na kujifunza namna ambavyo teknolojia inafanya kazi katika sekta ya kilimo na mifugo na kuweza kuleta tija kwa wakulima na wafugaji katika uzalishaji kwajili ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mhe. Chongolo ameyasema hayo alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwaajili ya kujione na kujifunza mambo mbalimbali yanayopatikana katika banda hilo kwenye maonesho ya Nanenene Nyanda za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale Mkoa wa Mbeya.
“Kwenye maonyesho haya sisi tunapita kwanza kujifunza lakini pia kujionea namna ambavyo teknologia iliyoboreshwa inavyoendelea kufanya kazi kwenye maeneo ya kilimo , uvuvi na ufugaji kwaajili ya kuongeza tija kwa wananchi”ameseme Chongolo
Aidha Mhe .Chongolo ametembelea na kujionea bidhaa mbalimbali za kilimo ikiwa ni pamoja na mbegu za mazao mbalimbali, mazao ya misitu ikiwemo asali, masalia ya wanyama pori kama vile Ngozi ya Mamba, fuvu la kichwa cha Tembo, viatu vya ngozi pamoja na makundi mbalimbali ya vyakula na vichangamshi kwaajili ya watoto na mambo mengine mengi.
Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeungana na Halmashauri nyingine za mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa Songwe na Katavi) katika sherehe za Maonesho ya nanenane mwaka 2024 huku kauli mbiu ya maonesho hayo ikiwa ni “Chagua viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo ya kilimo na Mifugo”
Afisa wanyamapori bi Simphrose Kavishe kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chunya akielezea kuhusu ngozi ya Mamba kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Daniel Chongolo alipotembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya katika maonyenye ya nane nane Nyanda za juu Kusini yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
Afisa Misitu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chunya bi Rehema Mwabulambo akielezea mazao mbalimbali ya misitu ikiwemo zao la asali kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe.Daniel Chongolo wakati alipotembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwenye maonesho ya nane nane Nyanda za juu kusini.
Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya bi Rehema Hiluka akielezea juu umuhimu wa vichangamshi kwa wototo pamoja na makundi ya vyakula kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwenye maonesho ya nane nane Nyanda za juu kusini Mkoani mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mh. Daniel Chongolo akipata melezo kutoka kwa Afisa kilimo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Lameck Matukuru juu ya mazao mbalimbali yaliyopo kwenye maonyesho wakati alipotembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwenye maonyesho ya nane nane katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.