Mkuu wa wilaya ya Chunya Bi.Meryprisca Mahundi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi. Sophia J. Kumbuli siku ya tarehe 01/02/2019, wametoa sisitizo na kugawa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo katika stendi ya mabasi Chunya.
Baada ya afisa Biashara wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg Mathias Mbele kutoa elimu ya kina kuhusu vitambulisho vya wajasiria mali wadogo, Mkuu wa wilaya amesema yafuatayo:
"Ukiwa kama mjasiriamali mdogo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya unatakiwa kuchangia tsh 20,000/= kwa ajili ya mapato ya taifa. Kitambulisho hicho kitakufanya uwe huru kufanya biashara ndogondogo katika nchi nzima ya Tanzania. Kitambulisho hicho kinahusisha mwendesha bodaboda, mpigadebe na shughuli nyingine stahiki” Mahundi.
Baadaye mkuu wa wilaya ya Chunya akatoa kitambulisho kwa mmoja kati ya wajasiriamali wadogo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.