Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya chunya Mhe. Bosco Mwanginde kwa kushirikia na wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wilaya ya chunya, viongozi wa kijiji cha Shogo na Askari wa jeshi la Akiba (Migambo) wamefanya oparesheni ya kuangamiza matanuri ya Mkaa
Oparesheni hiyo imefanyika Jana April 17, 2023 katika kitongoji cha Kambikatoto kilichopo kijiji cha Shoga kata ya Sangambi, jumla ya matanuri 10 ambayo tayari yalikuwa yamepangwa kwa ajili ya kuchoma mkaa yameteketezwa.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mhe, Mwanginde amesema baraza la madiwan kupitia kikao chake cha robo ya pili waliazimia kuwa ukataji holela wa mkaa wilayani chunya usitishwe kwani unahatarisha kupotea kwa viumbe hai na uharibifu wa mazingira
“Baraza liliazimia kwa kauli moja kwamba sasa ni marufuku kwa mtu Kuchoma mkaa ndani ya wilaya ya chunya bila ya utaratibu” alisema Mhe. Mwanginde
Pia Mwangine amewa taka wananchi wote wa wilaya ya chunya kuacha maramoja shughuli za uchomaji wa mkaa ndani ya wilaya bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.
“Kuanzia sasa ni marufuku mtu kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa katika maeneo haya hata maeneo mengine bila ya kupata kibali kutoka Ofisi za TFS” alisema Mwanginde
Aidha Mwanginde amewataka viongozi wa wilaya ya chunya kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo kwanguvu zote ili kuokoa na kunusuru mazingira ambayo yanaharibiwa na ukataji holela wa miti kwa ajili yaUchomaji wa Mkaa.
Hili sio zoezi la Mwenyekiti peke yake viongozi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya tuwe tayari kushirikiana na wenzetu wa TFS ili tuweze kutokomeza kabisa ukataji holela wa Miti.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.