Serikali na wadau mbalimbali wakiwa katika harakati za kukabiliana na tatizo la ushoroba nchini, Afisa mipango na uratibu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Janeth Mwaigoga kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji amewapokea wawakilishi wa mashirika ya TDFT, ADAP na TML (UPENDO HONEY) waliofika wilayani humo, Tayari kwa kuanza kuendeleza Juhudi za kuokoa Ushoroba wa wanyama ulio hatarini kutokana na shughuli za kibinadamu zinazovamia maeneo hayo.
Akizungumza mapema November 3, 2023, katika Hafla ya kutambulisha mradi unaoitwa USAID/TUHIFADHI MALIASILI iliyofanyika katika ukumbi wa Omary City Hotel, amewataka wakuu wa Idara na vitengo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Chunya kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa watendaji wa Mashirika hayo wakati wa utekelezaji wa mradi huo, ili kufanikia lengo lililo kusudiwa katika mradi unaoanza utakelezaji wake hivi karibuni na unaofadhiriwa na watu wa Marekani (USAID).
“Wakuu wa Idara na Vitengo mlioalikwa kwenye shughuli hii na wale ambao mtatakiwa kushiriki moja kwa moja kwenye utekelezaji wa mradi huu kipindi chote cha mradi hakikisheni mnapatikana kwa wakati na mnatoa usaidizi unaotakiwa na kwa kufanya hivyo mtasaidia azma ya uwepo wa mradi”.
Wakati akiwasilisha mada ya namna shirika la TDFT litakavyo shiriki katika utekelezaji wa mradi, meneja mradi Ndugu Samson Mwakihaba amesema Shirika la TDFT linalenga kuwafikia wananchi katika makundi mbalimbali wakiwepo vijana pamoja na wanafunzi ili kuhakikisha wanapata Elimu ya kutosha kuhusu uhifadhi wa ushoroba huo huku akiamini wananchi wanaweza kujihusisha na uharibifu wa mazingira ya ushoroba kutokana na kukosa ufahamu hivyo tumeomba ninyi viongozi wa serikali kwa mpate uelewa na pia mtaendeleza mradi baada ya sisi kumaliza muda wetu.
“Sisi tunaishia miaka miwili tu lakini tumewaita ninyi ili muulewe mradi kwa ujumla wake na pia muendeleze shughuli za mradi pindi sisi tutakapokuwa tumemaliza muda wetu wa kutekeleza mradi huu huku lengo la ninyi kuendleza shughuli za mradi huu likiwa ni kutimiza azma ya serikali la kuhakikisha tunahifadhi na kutunza mazingira kwa ujumla wake ikiwepo Mapitio ya wanyama" Amesema Ndg. Mwakihaba.
Kwa upande wa kampuni ya UPENDO HONEY wao katika mradi huu watajikita katika kuwajengea uwezo wananchi wanufaika wa mradi wa uzalishaji wa asali bora , kuhamasisha wanawake kushiriki katika zoezi la uzalishaji wa asali ikiwa ni sehemu ya kujiongezea kipato lakini pia kufanya mafunzo na mahusiano ya jamii na soko la asali maeneo mengine nje ya Tanzania lakini pia kutoa ufadhili kwa masomo yanayohusu Nyuki kwa wanafunzi sita katika Chuo cha Nyuki Tabora.
Wakati Shirika la ADAP watashiriki kwenye mradi kwa kuhakikisha Shoroba zinatambuliwa kwa kutoa hati miliki huku wakihakikisha wananchi wanaoishi karibu na shoroba hizo wanapata hati miliki za aridhi zao ili kuzuia wao kujiongezea maeneo kwa upande wa shoroba, watasimamia ukamilishaji wa mpango wa matumizi bora ya aridhi , wataimarisha ushiriki wa jamii katika kulinda Ikolojia na shughuli nyinginezo.
Mradi wa Tuhifadhi maliasili unafadhiliwa na watu wa Marekani, kwa wilaya ya Chunya utatekelezwa katika kata za Mafyeko, Kambikatoto, Mtanila, Lualaje na Matwiga ambapo vijiji saba vitanufaika na mradi huo na utadumu kwa miaka miwili kuanzia mwaka huu 2023 na kutamatika mwaka 2025.
Bwana Mwakihaba meneja Mradi wa shirika la TDFT unaofadhiriwa na watu wa Marekani (USAID) akiwasili mada mbele ya viongozi na wadau mbalimbali wilayani Chunya wakati wa utambulisho wa Mradi wa Tuhifadhi Maliasili wilayani Chunya
Meneja mradi wa Shirika la ADAP ndugu Romanus Mwakimata akiwasilisha namna shirika la ADAP litakavyoshiriki katika mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaotaraji kuanza kutekelezwa hivi karibu wilayani Chunya
Mkurugenzi mtendaji uzalishaji wa kampuni ya TML (UPENDO HONEY) BI Isabell Von Oerten akifafanua namna ambavyo kampuni hiyo itakavyoshiriki katika mradi wa Tuhifadhi Maliasili na namna ambavyo wananchi wa Chunya watafaidika kupitia Kampuni hiyo wakati wa utambulisho wa Mradi huo
Kaimu afisa Elimu awali na Msingi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mw John Gwimile akichangia Jambo wakati wa utambulisho wa mradi wa Tuhifadhi Maliasili unafadhiriwa na USAID unataraji kutekelezwa kuanzia mwaka huu wilayani Chunya
Washiriki toka Taasisi za Serikali, taasisi binafsi na Asasi za kirai wakiwa wanaendelea kufuatilia utambulisho wa Mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaotaraji kutekelezwa wilayani Chunya kuanzia mwaka huu, na anayewasilisha mbele ni meneja wa Mradi kutoka shirika la TDFT Ndugu Samson Mwakihaba
Washiriki waliohudhuria kutambulishwa kwa mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaofadhiriwa na watu wa Marekani (USAID) wakiwa kwenye picha ya Pamoja baada ya kutamatika kwa zoezi la utambulisho wa Mradi huo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.