Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Chunya ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Mheshimiwa Rehema Madusa leo tarehe 28/11/2017 amefunga rasmi mafunzo ya mgambo
Vijana hao pia katika risala yao walimshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa kuwa nao kipindi chote cha mafunzo nawalimuomba pia awape kipaumbele pindi ajira za kazi zitakapojitokeza.
Akihutubia katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya aliwapongeza wahitimu wote na kuwaahidi kuwa serikali ya wilaya ipo pamoja nao na atayafanyia kazi maombi yao.
Mbali na hilo Mheshimiwa Madusa aliwataka vijana hao kutumia mafunzo waliyoyapata vizuri na sio vinginevyo.Pia hakuacha kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira pamoja kuwapeleka watoto wao shule na kuwapatia huduma ya chakula.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.