Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Albert Chalamila amefanya ziara ya siku tatu katika wilaya ya Chunya ambapo aliweza kutembelea migodi ya dhahabu, kuwatembelea waendeha bodaboda na kuwapa elimu juu ya kazi zao za udereva wa pikipiki pamoja na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali.
Katika ziara zote hizo kwenye migodi ya dhahabu, aliwasisitiza Watanzania waliopo katika migodi hiyo kuwa wazalendo kwa nchi kwa kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa za watu wanaotorosha madini hali ambayo inaikosesha serikali mapato. Kwa upande mwingine aliwaambia wamiliki wa migodi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na sharia za nchi.
Akiwa katika mikutano yake ya hadhara, Ndg. Chalamila alisikiliza kero mbalimbali za wananchi ambapo zingine alizipatia ufumbuzi na zingine kuahidi atazishughulikia akishirikiana Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na ofisi ya Mbunge.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.