Afisa tawala Wilaya ya Chunya Bi Semwano Mlawa amewataka walimu wakuu, wakuu wa shule , walimu wa takwimu na walimu wa Tehama walioshiriki mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni School Information System (SIS) kwenda kuwa mabalozi wa mfumo huo kwa walimu wengine ili kurahisisha utekelezaji wa majukum yao lakini pia kuendana na kasi ya teknolojia ya sasa inayotumia mifumo mbalimbali ya kidigitali
Kauli hiyo ameizungumza leo tarehe 14/01/2025 wakati akifungua mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni (SIS) yaliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
“ Kwadunia ya sasa kwa namna yoyote ile hatuwezi kuepukana na masuala ya mifumo tutake tusitake mifumo ipo na itaendelea kuwepo kwasababu kizazi tunachoendelea nacho ni kizazi cha tofauti, kuna mifumo mingi sana kwahiyo ni lazima tuendane na mifumo ya kidunia inavyoenda, hivyo walimu mliohudhuria mafunzo haya mkawe mabalozi kwa walimu wengine Shuleni mnakotoka” amesema Bi Semwano
Aidha ameongeza kuwa mfumo huu utasaidia kurahisisha ukusanyaji wa taarifa kwa ujumla kwa wanafunzi na walimu hivyo kumuwezesha mwalimu kutekeleza majukumu mengi kwa wakati mfupi na kwa urahisi Zaidi kwa kutumia mfumo kukusanya taarifa za Walimu na wnafunzi.
Afisa elimu vifaaa na takwimu Msingi Mwl Gerald Shitindi amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu kuujua mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni School Information system ( SIS) na kwenda kuutumia kwaajili ya kuingiza taarifa mbalimbali za walimu na wanafunzi kwa Shule za Msingi na Sekondari ikiwa ni pamoja na mahudhurio, ratiba za vipindi, uhamisho na taarifa zingine.
Wakizungumza kwa niaba ya walimu wengine Mwl.Atanasi Mwakapelila na Mwl Levetina Mbilinyi wamesema kuwa mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni unarahisisha utekelezaji wa majukumu yao lakini pia mwalimu anaweza kufanya kazi kubwa kwa muda mchache tofauti na ilivokuwa awali kabla ya mfumo.
Mafunzo hayo ya Mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni yatadumu kwa muda wa siku mbili leo tarehe 14 na tarehe 15 kwa walimu wakuu wakuu wa shule , Walimu wa Tehema na walimu wa Takwimu kwa Shule za msingi na Sekondari iili kuwawezesha walimu hao kuutumia mfumo hou ifikapo tarehe 15/02/2026 na kuendelea.

Afisa elimu vifaa na Takwim Mwl Gerald Shitindi akieasilisha baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni wakati wa mafunzo kwa walimu yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

Afisa Tehama wilaya ya Chunya ndugu Mswaki Maganga akiwasilisha maada kuhusu ujazaji wa alama za wanafunzi kwenye mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni (SIS). katika ukumbi wa mikutano wa Sapanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

Walimu wakuu, Wakuu wa Shule , Walimu wa takwimu na walimu wa Tehama wakifuatilia Mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa Shuleni (SIS) katika ukumbi wa mikutano wa Sapanjo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.