Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe.Bosco Said Mwanginde amewataka wajumbe wa kikao cha wadau wa masuala ya ardhii kuhakikisha elimu wanayokuwa wameipata katika Mafunzo mbalimbali wanaitumia katika kuelimisha wananchi wengine kuhusu ardhi katika maeneo wanayotoka
Kauli hiyo ameitoa tarehe 28 februari 2024 wakati akifungua kikao cha wadau wa ardhi kilicho andaliwa na taasisi ya MIICO inayotekeleza mradi wa Uendelezaji wa upatikanaji wa ardhi bora kwa wazalishaji wadogo Nyanda za juu kusini mwa Tanzania ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya katika kata ya Sangambi na Upendo kilichoketi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya uliopo jengo jipya la utawala
“Kaitumieni elimu mnayoipata huko mnakokwenda na kwenye majukwaa yenu wajue nini mnakifanya,madiwani mliopo hapa kule mnakotoka kunakuwaga na migogoro ya masuala ya ardhi mkajitahidi kuelimisha watendaji wa kata na nyinyi pia mkasimamie haya mtakayoyapata huko kwenye maeneo yenu”alisema Mhe Mwanginde.
Glory Mdindile Afisa mradi kutoka MIICO akieleza malengo ya Mkutano pamoja na mpango kazi wa taasisi hiyo amesema kuwa lengo kuu ni kutammbulisha mradi katika awamu ya nne ya utekelezaji lakini pia kushirikishana mipango kazi na wadau wengine kwenye masuala ya ardhi ikiwa ni pamoja na kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau katika masuala ya ardhi.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Athuman Bamba ambaye ni mwanasheria wa Wilaya ameishukuru taasisi ya MIICO kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya arhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya na kutoa rai kwa watendaji na wenyeviti wa vijiji wa maeneo husika kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa taasisi hiyo.
Afisa kilimo na Mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ndugu Cuthbert Mwinuka ameeleza mipango mikakati iliyowekwa na Halmashauri katika kupambana na changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashamba ya lanchi kwaajili ya wafugaji lakini pia kuendelea kuwaelimisha wananchi kila mmoja kuheshimu mipaka yake kulingana na jinsi maeneo yalivyotengwa kupitia mpango wa matumizi bora ya ardhi
Faraja Kyando mwakilishi wa wakulima Sangambi ,Reonald Manyesha Mwenyekiti wa wachimba madini Mkoa wa Mbeya na Shangai Rapoy mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Wilaya ya Chunya ni miongoni wa wadau waliowasilisha mambo mbalimbali wanazofanya pamoja na kueleza changamoto mbalimbali wanazo kabiliananazo katika masuala ya ardhi kubwa ikiwa ni migogoro ya ardhi baina ya wafugaji , wakulima pamoja na wachimbaji wa madini katika maeneo yao
Kikao hicho kimehusisha wadau mbalimbali wakiwemo waheshimiwa madiwani wa maeneo unakotekelezwa mradi ,wadau wa azaki,wakulima na wafugaji, wachimbaji wa madini wakuu wa idara mbalimbali ,watendaji kata na wenyeviti wa vijiji nakuazimia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwaomba watu wa madini wasitoe lesseni mpaka wafike eneo husika na kujiridhisha kama halina Migogoro yoyote.
Gloria Mdindile Afisa mradi kutoka taasisi ya MIICO akiwasilisha malengo na mpangokazi Shirika kwa awamu ya nne ya utekelezaji wa mradi kwa wadau walioshiriki kikao hicho kilichoketi katika Ukumbi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Chunya
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya akitoa neno la Shukrani kwa Shirika la MIICO linalotekeleza mradi wa ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ambako mradi huo unatekelezwa
Afisa kilimo na Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Cuthbert Mwinuka akielezea mikakati mbalimbali ya Halmashauri katika kutatua changamoto mbalimbali juu ya wakulima nawakati wa kikao cha wadau wa MIICO kilicho keti katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Mwenyekiti wa wachimbaji madini Mkoa wa Mbeya ndugu Reonald Manyesha akichangia juu ya changamoto ya utaratibu unaotumika kutoa lesseni unavyochangia migogoro ya ardhi kwenye kikao kilicho andaliwa natShirika la MIICO kilicho keti katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Wadau mbalimbali walioshiriki kikao kilichoandaliwa na Shirika la Miico kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali kuhusu ardhi pamoja na kutambulisha mradi wa ardhi awamu ya nne ya utekelezaki
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.