Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wameendelea kunufaika na uwepo wa minada ya Mifugo iliyoboreshwa kwaajili ya biashara ya kuuza na kununua mifugo kwa bei inayoendana na mifugo hiyo lakini pia kumwezesha mnunuzi kununua mifugo ambayo ni halali na imekaguliwa ili kumlinda mlaji .
Ndugu Kinawanga Samhenda Mfugaji na ndugu Hamis Pauyole Mfanya biashara ya Nyama ya Ngombe mwamewashauri wafugaji wanaouza mifugo yao majumbambani kupeleka mifugo yao kwenye minada iliyotengwa na serikali kwani inawasaidia wao kama wafugaji kuuza mifugo yao kwa utaratibu na kwa bei shindani kulingana na mifugo yao kwani wanaouza Mifugo yao majumbani wanauza kwa bei ndogo kwasababu ya kukosa ushindani wa soko.
Afisa mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dkt Benedicto Matogo akizungumza na wandishi wa Habari kwenye Mnada wa Mapogolo kata ya Chokaa amesema kuwa uwepo wa minada umesaidia kuwaleta wafugaji pamoja, kuleta ushindani wa wanunuzi jambo ambalo humletea faida mfugaji lakini pia minada hiyo imerahisha ukusanyaji wa mapato yanayotkana na biashara hiyo ya mifugo
“Minada hii iliyoboreshwa imekuwa nguzo kubwa ya uchumi wa serikali , wafugaji pamoja na wafanyabiashara wa mifugo kwani imekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa Serikali , wafugaji na wafanyabiashara minada imepelekea uwepo wa soko lenye ushindani wa bei kutokana na ujio wa wafanyabiashara wengi wanaotoka maeneo tofauti tofauti na kumwezesha mfugaji kuuza mifugo yake kwa bei inayoendana na thamani ya mfugo’’ alisema Dkt Matogo
Naye afisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Lodrick Mwakisole ametoa wito kwa wanawake na vijana kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika maeneo ya Minada ya Mifugo ikiwa ni pamoja na kuuza na kununua mifugo, kuuza bidhaa mbalimbali kama vile chakula vinywaji na biashara nyingine kwani soko ni la uhakika kutokana na uwepo wa watu wengi wanaofika eneo la Mnada
‘’Kuna fursa kubwa kwa vijana na kinamama katika sekta ya mifugo kama unenepeshaji wa mifugo, vyakula vya mifugo lakini si hivyo tu kwenye eneo la mnada kuna biashara nyingine nyingi ambazo zinafanyika kama vile kuuza vyakula, nguo na biashara zingine’’ alisema Mwakisole
Mfugaji Kinawanga Samhenda na Mfanya biashara ya Nyama ya Ngombe ndugu Hamis Pauyole mwamewashauri wafugaji wanaouza mifugo yao majumbambani kupeleka mifugo yao kwenye minada iliyotengwa na serikali kwani inawasaidia wao kama wafugaji kuuza mifugo yao kwa utaratibu na kwa bei shindani kulingana na mifugo yao kwani wanaouza mifugo yao majumbani wanauza kwa bei ndogo kwasababu ya kukosa ushindani wa soko.
Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ina minada ya Mifugo miwili (2) iliyoboreshwa na Mnada wa Sipa na Mnada wa Mapogolo pamoja na Minada midogo midogo 13 ambayo hufanyika kila mwezi mara moja na kuwawezesha wafugaji na wafanyabiashara kuuza na kununua mifugo pamoja na bidhaa mbalimbali ambazo huuzwa katika meeneo hayo ya Minada ili kujipatia kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa.
Ndugu Kinawanga Samhenda Mfugaji kutoka kijiji cha Sangambi akiwa katika Mnada wa Mapogolo uliopo kata ya Chokaa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwaajili ya kuuza Mifugo yake.
Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dkt Benedicto Matogo akizungumza na wanahabari wakati wa Mnada wa Mifugo uliofanyika katika Mnada wa Mapogolo kata ya Chokaa
Afisa biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Lodrick Mwakisole akielezea fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye Minada ya Mifugo wakati alipokuwa kwenye Mnada wa Mifugo wa Mapogolo uliopo kata ya Chokaa.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.