MKUU wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Z. Homera ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kuhakikisha wanapeleka fedha kukamilisha ujenzi wa kituo cha Afya Ifumbo ili kiweze kutoa huduma kwa wananchi.
Homera ametoa maagizo hayo aliposhiriki katika kikao maalam cha Baraza la Hoja ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ina jumla ya hoja 17 ambazo hazijapatiwa majibu.
“Tafuteni milioni 50 pelekeni pale na kama hamjatenga kwenye bajeti tafuteni hela ziende na sisi tunachotaka katika moja ya hoja zitakazojifunga kwa mwaka ujao wa fedha na hiyo hoja ya kituo cha afya Ifumbo kiwe kimeshakamilika” amesema Homera
Homera ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kufanya uhamishaji wa fedha ili kuweza kuhakikisha wanapeleka hela kwenye kituo hicho.
“Fanyeni reallocation {uhamishaji} pelekeni milioni 50 kwenye hicho kituo hayo ni maelekezo nikifika tena hapa nikakuta hamjapeleka hatutaelewana,” alisema Homera.
Homera aliongeza kusema kuwa, wananchi wa Kata ya Ifimbo wanapata sana shida kufuta huduma za afya wanatembea zaidi ya kilometa 35 kupata huduma za afya katika hospitali ya wilaya.
“Mama na mtoto wanapoteza maisha yao kwa kushindwa kufika katika Hospitali ya Wilaya, wanafia njiani na sisi tumo humu ndani Madiwani, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na wataalam tunashindwa kutafuta milioni 50”
Pia Homera aliongeza kwa kusema kwa kuwa wananchi wa Kata ya Ifumbo wanapata shida, hakuna haja ya kuchelewa, Halmashauri itafute fedha na kupeleka ili kukamilisha ujenzi wa hicho kituo.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Homera ameutaka uongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanawashirikisha waheshimiwa madiwani katika miradi yote inayotekelezwa na wafahamishwe kiasi cha fedha kinachotolewa.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Ifumbo, Mh. Weston Mpilya amesema ujenzi wa kituo cha afya Ifumbo ulianza tangu mwaka 2016 na mpaka sasa bado hakijakamilika kitu ambacho kinasababisha wananchi kupata adha ya huduma za afya.
“Jiografia ya eneo letu mpaka tunaifikia Hospitali ya Wilaya ni umbali mrefu sana na miundombinu ya barabara sio mizuri na kusababisha watu kupoteza maisha wakifuata huduma za afya,” alisema Mpilya.
Hamlashauri ya wilaya ya Chunya katika mwaka 2020/2021 ilitekeleza shuguli mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea wananchi wake maendeleo
Shughuli zilizofanyika zililenga kuimarisha ustawi wa wananchi wa chunya ili wajiletee maendeleo, shughuli zote zilifanyika kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ya serikali katika kuhakikisha matumizi ya rasilimali watu, fedha na rasilimali zilizopo katika halmashauri zinatumika kwa kuzingatia sheria.
Katika ukaguzi wa matumizi ya fedha na rasilimali kwa mwaka wa 2020/2021, halmashauri ya wilaya ya chunya imepata Hati inayoridhisha, Kwa mwaka huo halmashauri ilikuwa na hoja 47 ambapo zilikuwa zimetolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, hoja thelathini {30} zimefungwa na hoja Kumi na Saba {17} zinaendelea kutekelezwa
Aidha halmashauri ilikuwa na maagizo Saba {7} ya kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, maagizo matatu {3} yametekelezwa na maagizo manne bado yanaendelea kutekelezwa.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mh Mayeka S. Mayeka Akizungumza kwenye kikao maalumu cha Baraza la Hoja
Wahshimiwa Madiwani kutoka kata mbalimbali za halmashauri ya wilaya ya chunya wakiwa kwenye kikao maalumu cha Baraza la Hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Halmashauri
Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wakifuatilia kwa makini kikao maalumu cha Baraza la Hoja
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mh. Bosco Mwanginde ambaye ni Diwani wa kata ya Mbugani akiwasilisha hoja kwenye kikao maalumu cha Baraza la Hoja
Kaimu Mkurugenzi Ndg Curthbert Mwinuka Akifafanua jambo kwenye Kikao maalumu cha Baraza la Hoja za Ukaguzi wa Hesabu za Halmashauri
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.