Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amewataka watendaji kusimamia suala la usafi na kulipa kipaumbele hasa kipindi hiki cha masika ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kutokea kutokana na uchafu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuna kuwa na madampo ya kumwaga taka na si kutupa taka hovyo pamoja na kuendelea kusimamia vizuri miradi ya maendeleo katika maeneo yao iweze kutekelezwa kwa ubora na viwango
Hayo ameyasema leo Desemba 3/2024 wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Tathimini ya Lishe ngazi ya kata kilichoketi katika Ukumbi wa Dadi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
Mhe Batenga amezitaka kata ambazo hazijafikia malengo katika utekelezaji wa afua za lishe kuhakikisha wanaongeza juhudu na ufwatiliaji ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa na kuvuka lengo hilo jambo litakaloifanya Halmashauri iendelee kufanya vizuri Zaidi katika masuala ya lishe.
Aidha Mhe. Batenga ametoa pongezi kwa watendaji wa kata wa kusimamia vizuri Uchaguzi wa serikali za mitaa katika maeneo yao hali iliyochangia uchaguzi kuisha kwa usalama na Amani na hali hiyo ni kutokana na utendaji kazi mzuri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wananchi wake .
“Kufanikiwa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kumekuja kutokana na wananchi kukubali utendaji kazi wa serikali yao yani mimi pamoja na ninyi hivyo tuendelee kujituma, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuwasikiliza wananchi wetu sio ninyi tu hii ni pamoja na taasisi zingine tunazofanyanazo kazi”Amesema Mhe.Batenga.
Naye katibu tawala wa Wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero ametoa rai kwa Watendaji wanapokuwa wanagawa maeneo kwa wananchi kukumbuka kutenga maeneo kwaajili ya taasisi ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza pale ambapo taasisi inauhitaji wa eneo kwaajili ya kuhudumia wananchi alafu eneo linakuwa hamna.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Wakili Athuman Bamba katibu wa kikao hicho ametaka watendaji wa kata na vijiji kujiandaa na kushiriki kikamilifu maadhimisho ya siku ya Uhuru ambapo Maadhimisho hayo yataadhimishwa kwa kutoa elimu kwa wenyeviti na wajumbe wa Halmashauri za vijiji yatakayofanyika kwa tarafa zote mbili, tarafa ya kiwanja na tarafa ya kipembawe kutoka kwa wataalam mbalimbali Wilaya ya Chunya ili kuwajengea uwezo wa namna ya kutekeleza vyema majukum yao.
Kaimu Afisa lishe Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Simoni Mayala amewataka watendaji kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kusimamia masuala ya Lishe katika kata zao kama ambavyo walisaini Mkataba wa lishe ikiwa ni pamoja na kutuma taarifa za utekelezaji kwa muda uliopangwa lakini pia kutoa ushirikiano changamoto yoyote inapojitokeza ili iweze kutafutiwa ufumbuzi.
Kikao cha tathimini ya Lishe robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya , Katibu tawala, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Maafisa Utumishi, Watendaji wa kata na Waratibu elimu kata kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa afua ya lishe kwa kipindi cha robo pamoja na kujadili changamoto mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe.Mbaraka Alhaji Batenga akizungumza na watendaji kata pamoja na waratibu elimu kata wakati wa kikao cha tathimini ya lishe ngazi ya kata kilichoketi katika ukumbi wa Dadi Wilayani Chunya
Katibu tawala wa Wilaya ya Chunya ndugu Anakleth Michombero akiwakumbusha watendaji kutenga maeneo ya taasisi pindi wanapogawa maeneo wakati wa kikao cha tathimini ya lishe ngazi ya kata kilichofanyika ukimbi wa Dadi Wilaya ya Chunya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya wakili Athuman Bamba akiwataka watendaji kuendelea kufuata na kutekeleza maagizo yanayotelewa katika kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na suala la lishe pamoja na ukusanyaji wa mapato.
Wajumbe wa kamati ya lishe ngazi ya kata wakifuatilia tathimini ya utekelezaji wa afua za lishe katika maeneo yao wakati wa kikao cha robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba .
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.