Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Mhe Bosco S. Mwanginde amewataka wazee waliopo wilayani Chunya kuacha kuwaogopa vijana ili kunusuru Taifa kwani Matokeo ya kuwaogopa vijana ni uharibifu na mmomonyoko wa maadili uliopo sasa ambao ni hatari kwa Taifa la sasa na hata kwa Taifa la Kesho.
.
Mhe Mwanginde ametoa kauli hiyo leo tarehe 1/10/2023 wakati akizungumza na wazee waliokusanyika kuadhimisha siku ya wazee duniani ambapo kwa wilaya ya Chunya maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) ambapo Mhe Mwanginde alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
“Wazee mnatuogopa vijana wenu jambo ambalo ni hatari na matokeo yake ni uharibifu huu wa maadili uliopo, hivyo ili turekebishe maadili ya Taifa hili lazima wazee muache kutuogopa sisi vijana, mzungumze nasi mtukemea kwa ukali kama wazee wetu wa zamani walivyokuwa wanafanya kwenu. Na kama mnaona kuna eneo mambo hayaendi vizuri maana yake kuna eneo wazee hamjakaa sawa na hamjafanya kazi yenu. kwa mfano, Ni mzee gani amefika ofisini kwangu kunishauri namna sahihi ya kuiongoza Halmashauri hii na sikumsikiliza? Je wazee wa zamani hawakukemea viongozi wazembe na wasiozingatia maadili ya kazi?” alihoji Mhe Mwanginde.
Aidha Mhe Mwanginde ameshauri katika maadhimisho yajayo lazima waalikwe vijana ili mausia na maonyo ambayo inawezekana hawajapewa na wazazi wao basi kupitia maadhimisho ya siku ya wazee kama haya, busara na hekima kutoka kwa wazee wengine zitawasaidia kutekeleza majukumu yao na kubadiri mwelekeo wao mbaya kama watakuwa na mwelekeo ambao haufai kwa jamii na Taifa kwa ujumla wake.
“Maadhimisho yajayo ya wazee lazima tuwaalike vijana ili tuwape maonyo ambayo yanaweza kuwasaidia katika maisha yao ya kawaida na inawezekana yako mambo kijana hajaambiwa na mzazi wake lakini kwa baraza kama hili inaweza kusaidia kupata mambo mengi muhimu sana maana tunao wazee kutoka maeneo mbalimbali jambo ambalo linafanya kila taaluma ipatikane kwenu wazee maana niyny ni hazina ya Taifa”.
Awali akitoa salamu za kata ya Itewe diwani wa kata hiyo Mhe Alex Kinyamagoha amesema maadhimisho ya siku ya wazee ni muhimu kwakuwa yamebeba mambo mengi ambayo ni maonyo na makalipio kwa vijana wa sasa ambao wengine ndio viongozi katika nyadhifa mbalimbali hivyo itawasaidia kutekeleza majukumu yao wakijua lipi ni zuri na limepata Baraka za wazee na lipi sio jambo sahihi kwa maslahi ya jamii anayoishi na pengine jamiii anayoiongoza kama yeye ni kiongozi.
Katibu wa baraza la wazee Donald Mwinanzi amewawakilisha wazee kwakueleza changamoto mbalimbali zinazo wakabili wazee ikiwa ni pamoja na ukosefu wa Bima kwa baadhi ya wazee, Upungufu wa dawa katika ameneo wanayoenda kutibiwa wazee,Kuachiwa wajukuu kuwalea, kutelekezwa na watoto wao wa kuwazaa, msongo wa mawazo pindi eanapokuwa wametelekezwa na watotio wao na changamoto ntinginezo hivyo kuitia hadhara hiyo katibu kwa niaba ya wazee ameomba serikali kushughulikia changamoto hizo.
Kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya afisa ustawi wa jamii Bi Lutiness Mbissa amesema adhima ya maadhimisho hayo ni kuwaleta wazee pamoja na kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo na kutafuta suluhu yake huku akisema serikali itaendelea kuwajali na kuwakumbuka wazee kwakuendelea kufanya mambo mbalimbali yanayojali ustawi wao.
Maadhimisho hayo yamehusisha upimaji wa afya kwa watu wote walio tayari kupima bila gharama zozote lakini mada mbalimbali zimewasilishwa na zimejadiliwa na washiriki wa maadhimisho hayo huku burudani mbalimbali zimesaidia kufurahisha na kuliwaza wazee wote waliojitokeza.
Diwani wa kata ya Itwe Mhe Alex Kinyamagoha akitoa salamu za kata ya Itwe mbele ya Mwenyeki wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambapo kwa wilaya ya CVhunya yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano Sapanjo leo
Mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya ya Chunya Mzee John Ilomo akizungumza Mbele ya Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wazee Duniani ambapo kiwilaya yamefanyika ukumbi wa mikutano Sapanjo
Katibu wa Afya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Chrispina Kasikiwe akizungumza Mbele ya Mgeni rasmi wakati wa Maadhimisho ya siku ya wazee Duniani
Afisa ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Lutiness Mbissa akizungumza Mbele ya Mgeni rasmi wakati wa Maadhimisho ya siku ya wazee Duniani iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo)
Katibu wa Baraza la Wazee (Mwenye koti jeusi) akisaidiwa na katibu msaidizi wa baraza hilo wakati akisoma Risala mbele ya Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wazee Duniani
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.