Wazir wa madini Mh. Doto Biteko amepiga marufuku uchimbaji wa madini kwenye mlima Kaputa uliopo wilayani Chunya kutokana na mgogoro uliopo baina ya mwekezaji Mazyele na wananchi. Mh.Waziri amefikia maamuzi hayo baada ya yeye mwenyewe kufika eneo la mlima huo ambao chanzo cha mgogoro huo ni wananchi kusema kwamba uchimbaji unafanyika kwenye maeneo ya makaburi na visima vya maji. Hata hivyo waziri aliona kwamba uchimabji ambao ulikuwa ukifanywa na mwekezaji haupo karibu na makaburi na visima vya maji ila wanaochimba karibu na makaburi ni wachimabji wadogo. Ili kumaliza mgogoro huo Mh. Waziri ameamua kusitisha uchimbaji wa madini katika mlima huo mpaka pale ambapo serikali itatoa maamuzi mengine.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.