Mbunge wa Jimbo la Chunya, Mheshimiwa Masache Kasaka ameizindua zahanati ya Godima iliyopo Kata ya Chokaa Wilaya ya Chunya.
Akizindua zahanati hiyo, Mhe Kasaka {Mb} amesema lengo ni kuhakikisha yale yote waliyoyaahidi kwa Wananchi wanayatizima ili kuwaletea maendeleo.
“Ndugu zangu wana Godima, leo tarehe 20.07.2022 imekuwa siku ya furaha kwetu, uzinduzi wa zahanati hii ina maana kwamba afya zetu zinaenda kuwa bora zaidi,” alisema Mhe. Kasaka.
Kasaka aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha miundombinu ya huduma za afya inaboreshwa kwa wananchi na kuwataka wataalamu wa zahanati ya Godima kutoa huduma stahiki kwa wanajamii.
Kadhalika Mhe. Kasaka {Mb} amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Godima kwa namna walivyojitoa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa zahanati hiyo kwa kutoa michango mbalimbali.
"Kwanza niwapongeze kwa namna ambavyo tumejitolea michango yetu mbalimbali mpaka kufikia hatua hii ilipofikia, ni vijiji vichache sana ambavyo vinaweza jitolea kama ambavyo nyinyi mmejitolea." Alisema Kasaka.
Mheshimiwa Kasaka aliongeza kwa kusema kuwa, ndani ya mwaka mmoja Wilaya ya Chunya kwenye sekta ya afya imefanikiwa kutekeleza ujenzi wa zahanati nane na vituo vya afya vitatu ambavyo vitaenda kuimarisha huduma ya afya kwa wananchi.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Chokaa Mhe. Samwel Raphael Komba, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ndg. Edward Righton Tengulaga, Kamati ya Halmashauri ya Kijiji pamoja na Wananchi wa kijiji cha Godima.
Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg. Edward Righton Tengulaga wakwanza Kushoto akifafanua jambo mbele ya Mhe. Masache Kasaka Mbunge wa jimbo la Lupa aliyevaa shati ya Kijani wakati wa Uzinduzi wa zahanati ya Kijiji cha Godima, kata ya Chokaa
Diwani wa kata ya Chokaa Mhe. Samweli Komba akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Godima waliojitokeza wakati wa Uzinduzi wa Zahanati ya kijiji hicho
Wananchi mbalimbali wa kijij cha Godima waliojitokeza kwenye hafla ya uzinduzi wa zahanati ya kijiji
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka aliyevaa shart lakijani sambamba na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndg. Edward Tengulaga wakikagua zahanati ya Godima kabla ya Uzinduzi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.