Mbunge wa jimbo la Lupa Mhe. Masache Njeru Kasaka amewataka waumini wa dini zote wilayani Chunya kuendelea kuombea Taifa ili Amani iliyopo iendelee kudumu zaidi jambo ambalo litasaidia serikali ilyopo madarakani kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi wake na wananchi mtaendelea kutekeleza majukumu yanu kwa shughuli halali za kujipatia kipato.
Mhe Masache ametoa rai hiyo mapema leo jumapili ya tarehe 1/10/2023 alipopata nafasi ya kuwasalimia waumini waliojihudhurisha kwa ibada wakati aliposhiriki ibada katika kanisa la Moraviani Tanzania ushirika wa Chunya
“Ndugu waumini niwaombe mwendelee kuliombea Taifa letu la Tanzania ili Amani iliyopo iendelee kudumu ndipo sisi watumishi wenu tutaendelea kuwatumikia kwa amani lakini pia ninyi mtaendelea kujishughulisha na shughuli zenu za Maendeleo kwa amani na niwakumbushe Amani haina dini, kabila wala kiwango cha pesa alicho nacho mtu hivyo jukumu la kuombea amani ni la wanaChunya wote bila kujali dini, kipato au eneo analo toka mtu.
Aidha Mhe Masache amechangia fedha kiasi cha shilingi Milioni moja katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kanisa hilo huku akisema kanisa ni moja ya mdau muhimu wa maendeleo si katika jimbo la Lupa tu bali pia Taifa lote la Tanzania maana sote ni mashahidi zipo shule, hospitali na miradi mingine mingi humilikiwa na taasisi za dini.
Kiongozi wa kanisa hilo Mchungaji Godfrey Tinha na Mchngaji Anyandwile Kajange ambaye ni mwenyekiti wa kanisa hilo Jimbo la Chunya wamemshukuru mbunge kuamua kutembelea kanisa hilo pamoja na mchango wake ambao umetowa kwa ajili ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kanisa hilo huku akiahidi kuendelea kuombea Taifa ili Amani iliyopo iendelee kudumu zaiidi na zaidi.
Mhe Masache yuko jimboni kwake tayari kwa ziara ya kukutana na wananchi ambayo inataraji kuanza kesho tarehe 2/10/2023 mpaka tarehe 11/10/2023 ili kutoa mrejesho wa Bunge la bajeti lililohitimishwa Juni 28, 2923, kusikiliza kero za wananchi na kutafuta suluhu ya kero hizo, kukutana na viongozi wa Chama na serikali katika vijiji, vitongozi na kata zao pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi wote ili kueleza utekelezaji wa Ilani kama alivyotumwa kuwasemea wananchi wa Chunya katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njeru Kasaka akisujudi ishara ya kupokea ama unyenyekevu wakati alipokuwa anakaribishwa kwenye Ibada aliposhiriki ibada ya leo katika Kanisa la Moraviani ushirika wa Chunya
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache wa kwanza kushoto akitambulishwa na Mchungaji Mwenyeji wa kanisa la Moraviani ushirika wa Chunya Mjini mapema leo aliposhiriki Ibada
Mvunge wa jimbo la Lupa Mhe Masache Kasaka wa kwanza kushoto akikabidhi fedha alizochangia katika kanisa hilo kwa lengo la kuchangia miradi ya kanisa hilo mapema leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.