Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe: MASACHE, NJERU KASAKA amesema kazi aliyotumwa na wananchi wa Chunya anaendelea kuitekeleza kwa weledi, ikiwa kuhakikisha miradi mbalimbali wilayani Chunya inatekelezwa na pia amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuitunza miradi inayojengwa wilayani humo ili idumu kwa muda mrefu
Mhe Masache amesema hayo alipokuwq akizungumza na wananchi waliojitokeza kupokea mitambo ya uchimbaji maji safi na salama wilayani Chunya ambapo Mhe Masache alimuwakilisha Naibu waziri wa Maji na umwagiliaji Mh: Maryprisca Mahundi kukabidhi mitambo hiyo
“Ndugu wananchi mitambo hii ya uchimbaji visima tunaiacha hapa Itumbi, msisubiri viongozi wa serikali wailinde na wala msisubiri askari polisi waje kuilindi, Ninyi muwe walinzi wa kwanza wa mitambo hii na mtoe ushirikiano pale utakapohitajika”
Naye Meneja wa RUWASA wilayani chunya Eng ISMAIL Nassor wakati akitoa taarifa ya upatikanaji wa maji wilayani chunya mbele ya Mhe Mbunge wa Jimbo la Lupa amesemsa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 ni kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama vijijini unafikia asilimia 85 lakini mpaka sasa hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika vijiji vya wilaya ya Chunya ni asilimia 47% hivyo mitambo hii itaongeza hali ya upatikanaji wa Maji maeneo mbalimbali wilayani Chunya
Aidha Mhe; Masache amewashukuru wananchi kwa utayari waliouonesha katika ziara ya Mkuu wa Mkoa Mhe Juma Zuberi Homera alipotembea Itumbi ambapo wananchi walichangia zaidi ya Shilingi Milioni Moja na huku Mkuu wa mkoa akiahidi milioni Mbili ili ujenzi wa Shule ya sekondari Masache uanze Itumbi ikiwa ni kuepukana na wanafunzi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya sekondari
Masache amesema kwakuwa ujenzi una hatua mbalimbali za ujenzi yeye kwa hatua hii ya kwanza amechangia milioni tano na amewataka wananchi kuwa tayari kwaajili ya harambee itakayopangwa hapo badaaye ili kufanyike changizo la ujenzi wa shule ya sekondari Masache ili kufikia Disemba mwaka huu shule iwe imekamilika na iko tayari kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2024
Katika hafla hiyo ya kukabidhi mitambo ya uchimbaji visima Mhe Masache aliongozana na viongozi Mbalimbali akiwepo Mbunge wa Jimbo la Kyela, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya wakiongozwa na Mweneyekiti wa Chama Ndugu Noel Chiwanga, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya pamoja na Viongozi wa RUWASA Wilaya na Mkoa
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe. Masache Kasaka akizungumza wakati wa hafla ya kupokea mitambo ya kuchimba visima wilayani Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.