Mkuu wa wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mhe Mbarak Alhaji Batenga ameagiza maeneo yote ya Serikali pamoja na Taasisi zote kupimwa kwa haraka sana na kupatiwa hati ili kuepuka uvamizi na migogoro inayojitokeza kati ya wananchi na serikali au serikali na wananchi jambo linaloweza kuathiri ushirikiano kati ya serikali na wananchi wake
Mhe Batenga ametoa agizo hilo leo tarehe 15/01/2024 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya serikali ya kitongoji cha Itumbi wakati alipoongoza msafara wa kamati ya usalama ya wilaya ikiamabatana na Meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) iliyokusudia kukagua ubovu wa miundombinu ya barabara ya Matundasi-Itumbi yenye urefu wa Kilomita kumi na mbili (12) na Barbara ya Mnazi mmoja- Sambilimwaya yenye urefu wa Kilomita tatu (3)
“Wiki ijayo mpima ardhi afike hapa katibu tawala simamia hilo ili maeneo yote ya serikali yapimwe na yapewe hati ili tuone uvamizi unatokea wapi na hii ndo itakuwa suluhisho la migogoro ya ardhi ndani ya wilaya ya Chunya na vijiji vyake”
Baadhi ya wananchi akiwepo Oden Mwakanyamale alieleza eneo la Makaburi kuuzwa na hakuna eneo la lingine lililotengwa kwaajili ya Makaburi, Twalibu Athuman yeye pia alieleza namna anavyosumbuliwa juu ya umiliki wa shamba lake wakati alinunua kihalali na mtu aliyemuuzia yupo na ushahidi upo
Aidha Mkuu wa wilaya ya Chunya amewataka wananchi wa wilaya ya Chunya kuendelea kuiamini serikali ya awamu ya sita chini Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwani ni sikivu na inawapenda wananchi wake na inatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma mbalimbali ili waendelee na shughuli za uzalishaji mali
Ziara ya Mkuu wa wilaya imekuja ili kutatua changamoto mbalimbali zilizobainika wakati wa ziara ya kamati ya Siasa ya wilaya ya Chunya ilipopita kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Chunya.
Katibu tawala wilaya ya Chunya Ndugu Anakleth Michombero akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha mkuu wa wilaya ya Chunya kuzungumza na wananchi wa Itumbi mapma leo kwenye mkutanouliofanyika viwanja vya ofisi ya kitongoji
Diwani wa kata ya Matundasi Mhe Kimo Choga akitoa salamu za kata mbele ya Mkuu wa wilaya katika mkutano uliofanyika Itumbi mapema leo
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Itumbi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chunya Mapema leo
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.