Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya Afisa Tawala wa Wilaya ya Chunya Bi Semwano Mlawa amewasilisha maelekezo manne (4) kwa Baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Makongolosi yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha swala la ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao unaimarishwa katika maeneo yote ikiwepo ulinzi shirikishi .
Maelekezo hayo yametolewa na Afisa Tawala akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chunya leo tarehe 13/02/2025 wakati wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Makongolosi la kuchagua Mwenyekiti , Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo na wenyeviti wa kamati mbalimbali katika Ukumbi wa Mama Mbwana Makongolosi Wilayani Chunya.
“Maelekezo 4 ya Mkuu wa Wilaya kwa baraza la mamlaka mji mdogo Makongolosi , jambo la kwanza ni suala la swala la usalama, jambo la pili ni ufwatiliaji wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti Shuleni, jambo la tatu ni usimamizi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yetu na jambo la nne tukasimamie ukusanyaji wa mapato na uratibu mzuri wa feda zinazokusanywa.” Amesema Bi Semwano
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chunya Ndugu Noel Chiwanga ametoa rai kwa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi kutatua kero mbalimbali za wananchi, kuoa haki na kuwahudumia Wananchi kwani wananchi wanamatarajio makubwa sana na viongozi wao.
“Toeni haki kwa wananchi kwani wananchi wanamatamanio na matarajio makubwa sana kwenu , naomba kero mbalimbali za wananchi mkazipunguze kwa kiasi kikubwa sana, sasa isije ikawa matarajio tofauti kwamba kuwepo kwako wewe ndio ikawa kero kwa wananchi” amesema Chiwanga
Nae Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHEDEMA) ndugu Yohana Mpamba ametoa msisitizo kwa baraza la mamlaka Mji mdogo Makongolosi kwenda kutenda haki kwa watu wote bila kubagua lakini pia kuiga mambo mazuri yanayofanywa na viongozi waliotangulia kwaajili ya maendeleo ya mamlaka na Wilaya ya Chunya kwa ujumla.
Kaim Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu John Maholani amawasihi baraza la mamlaka Mji mdogo Makongolosi kufanyakazi kwa bidii kwaajili kwani wana mamlaka makubwa ya katika kuiletea maendeleo Mamlaka ya mji mdogo Makongolosi , Halmashauri ya Wilyaya ya Chunya na Taifa kwa ujumla
Nae diwani wa kata ya Matundasi Mhe . Kimo Choga kwa niaba ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya mbali na kuwapongeza wenyeviti waliochagulia ametoa wito kwa viongozi hao kusimamia miongozo na taratibu za Mamlaka pamoja na kusimamia ukusanyaji mzuri wa mapato ambayo ndio dira ya maendeleo ya mamlaka ya mji mdoo wa makongolosi.
Balaza la Mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi la kuchagua Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Baraza hilo limeenda sambamba na kuchagua wenyeviti wa kamati mbalimbali za Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi limehudhuriwa na kamati ya Usalama Wilaya ya Chunya, Viongozi wa vyama vya Siasa wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chunya na mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi.
Afisa Tawala Wilaya ya Chunya Bi Semwano Mlawa akitoa maelekezo manne ya Mkuu wa Wilaya kwa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi katika Ukumbi wa Mikutano wa Mama Mbwana Makongolosi Wilayani Chunya.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndugu Noel Chiwanga akitoa salam za chama wakati wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi la kuchachugua viongozi wa baraza hilo na viongozi wa kamati mbalimbalii lililoketi katika Ukumbi wa Mama Mbwana wa Makongolosi Wilayani Chunya.
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi Ndugu Linus Mwanitega akitoa ufafanuzi juu ya uchaguzi wa viongozi wa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Ndugu John Maholani akitoa rai kwa wajumbe wa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi lililoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Mamam Mbwana Makongolosi Wilayani Chunya.
Wajumbe wa baraza la Mamlaka Mji Mdogo Makongolosi wakifuatilia agenda mbalimbali za kikao wakati wa baraza la kuchagua Viongozi wa baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi lililoketi katika Ukumbi wa Mikutano wa Mama Mbwana Makonolosi Wilayani Chunya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.