PICHANI: Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Chunya Mh. Bosco Mwanginde Akifungua Kikao Cha Baraza la Madiwani
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chunya limepitisha rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka 2022/2023, kwenye kikao kilichofanyika leo Januari 21, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Baraza hilo limepitisha rasimu ya bajeti yenye makisio yenye thamani ya shilingi bilioni 27,972,230,500.00 (bilioni) katika bajeti hiyo.
Mishahara kwenye bajeti hiyo imepangwa kuwa Sh.12,687,309,000,00, kiasi cha Sh. 11,190,782,900,00 kitaenda kwenye miradi ya maendeleo na mapato ya ndani ya Halmashauri yakiwa Sh. 1, 576,120,400.00.
Matumizi mengineyo ni Sh.4, 094, 138, 600, 00 na kufanya rasimu hiyo ya mpango na bajeti kwa mwaka 2022/2023 kuwa na jumla kuu ya Sh.bilioni 27,972,230,500.00.
Kwa upande mwingine, Madiwani hao wamewapongeza wataalamu wa Halmashauri kwa uandaaji mzuri wa bajeti hiyo ya 2022/2023 na kukiri kwamba bajeti hiyo ina mambo mengi mazuri kwa maendeleo ya wananchi.
Madiwani hao wameshauri pia Halmashauri hiyo kuendelea kuongeza nguvu na kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaisaidia Halmashauri kuweza kupata mapato kwa wingi, hatimaye kuweza kutekeleza vyema bajeti zinazopangwa na Halmashauri hiyo.
Mbunge wa jimbo la Lupa, Mh. Masache Njelu Kasaka amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa kuongoza na kuendesha vyema kikao cha Baraza la Madiwani na kupitisha rasimu ya bajeti kwa mwaka wa 2022/2023.
“Bajeti tuliyoipitisha hapa ndio mwelekeo wa Chunya ipi tunayoitaka, Mwenyekiti, Mkurugenzi pamoja na wataalamu kupitishwa kwa bajeti hii maana yake sasa jukumu kubwa linabaki mikononi mwenu, ikiwa ni usimamizi na utekelezaji”. Alisema Mh Masache.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mh. Mayeka Simon Mayeka, ameupongeza uongozi wa Halmashauri pamoja na Baraza la Madiwani kwa ukusanyaji mzuri wa mapato.
“Nakumbukwa mwaka uliopita kipindi kama hiki tulikuwa nyuma sana, lakini kwa hatua hii niliyoiona nawapongeza sana, kwa namna tunavyoenda nadhani tutakuwa na makusanyo mazuri na kuweza kupindukia asilimia zaidi ya 100”. Alisema Mh Mayeka.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Bw. Tamim Kambona, amewashukuru waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwa ushirikiano wanaompa yeye pamoja na watendaji wengine wa Halmashauri.
"Sisi kama watendaji wa Halmashauri tutahakikisha tunatekeleza yale yote ambayo ninyi mnatarajia yafanyike kwenye maeneo yenu.
“Mwenyekiti niwahakikishie madiwani sisi tutapeleka miradi kwenye kata zote bila kupendelea kata nyingine yoyote ile”. Alisema Kambona.
Akifunga kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mh.Bosco Mwanginde ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbugani, amesema kuwa bajeti hiyo ili iweze kutekelezwa kama ilivyopangwa inategemea ukusanyaji bora wa mapato kwa Halmashauri.
|
|
Afisa Mipango Wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi Janeth Mwaigoga Akiwasilisha Rasimu ya Bajeti kwa Mwaka 2022/2023 katika baraza la Madiwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bw Tamim Kambona akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wakati wa Kujadili rasimu ya Bajeti ya mwaka 2022/2023
Mh Mayeka Simon Mayeka Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani wakati ya Kujadili Rasimu ya Bajeti kwa Mwaka 2022/2023
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mh Masache Njelu Akizungumza kwenye kikako cha Baraza la Madiwani wakati wa kujadili Rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2022/2023
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.