Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mhe. Bosco Mwanginde amewataka watendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha fedha ambazo Halmashauri inadai kwa wadau zinafualiwa ili zilipwe haraka na baadaye pesa hizo zitumike maeneo mengine yenye uhitaji
Ametoa wito huo Agosti, 27 mwaka huu wakati wa kikao cha kujadili taarifa ya hesabu za mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya uliopo jengo jipya la utawala
“Tumeona kwenye taarifa hii, Halmashauri inadai shilingi milioni mia tatu na sabini na moja kutoka kwa wadau mbalimbali, fedha hii lazima ifuatiliwe ili ilipwe kwa wakati ili ipelekwe kutekeleze miradi ya maendeleo” alisema Mwainginde.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, Mhe. Mwanginde alisema magari yaliyochakaa pamoja na vifaa vyote vilivyoisha muda au kutokutumika vipigwe mnada ili fedha itakayopatikana itumike kwenye matumizi mengine ya Halmashauri.
Aidha Mhe Mwanginde aliwataka Madiwani na watumishi wa Halmashauri kuongeza ushirikiano baina yao na kufanya kazi kwa bidii hasa kwenye miradi ya maendeleo ambapo zaidi ya shilingi billion 3.3 sawa na asilimia 119 zimepelekwa kwenye miradi hiyo.
“Kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi ndio kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kujihakikishia cha kueleza wakati wa kuomba kura kwa wananchi Novemba 27 mwaka huu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na hata baadaye kwenye uchaguzi mkuu” alisisitiza Mwainginde.
Akisoma taarifa ya hesabu za mwaka 2023/2024, mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Rajabu Lingoni amesema, kwa miaka mitatu mfululizo yaani mwaka 2021/2022 Halmashauri ilishindwa kufikia malengo ya kukusanya mapato kwa asilimia 3, mwaka 2022/2023 ilipata ongezeko la asilimia 14 na mwaka huu 2023/2024 makusanyo yaliongezeka zaidi na kufikia ongezeko la asilimia 50.
“Mwaka 2021/2022 tulikusanya bilioni 5.3 ukilinganisha na makadirio ya kukusanya Bilioni 5.5, 2022/2023 tulikusanya bilioni 5.9 ukilinganisha na makadirio ya kukusanya Bilioni 5.2, 2023/2024 tulikusanya bilioni 9.8 ukilinganisha na makadirio ya kukusanya Bilioni 6.5,”alisema Lingoni.
Mwekahazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Rajabu Lingoni akisoma taarifa ya hesabu za mwaka 2023/2024 za Halmashauri kwenye kikao cha baraza la Waheshimiwa Madiwani la kujadili na kupisha hesabu hizo
Waheshimiwa madiwani wakipitia taarifa ya Hesabu za mwisho za mwaka 2023/2024 za Halmashauri ya Wilaya ya Chunya
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.