Maafisa waandikishaji wa Daftari la Mkazi wilaya ya Chunya watakiwa kuwa wazalendo na wenye kulipenda Taifa lao jambo litakalofanya wajitume kutekeleza jukumu la kuandikisha wapiga kura kwenye Daftari la Mkazi lililoko kwenye kitongoji husika ambalo litatumika wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 ambapo viongozi wa mbalimbali wa vijiiji na vitongoji wataachaguliwa
Akizungmza leo tarehe 08/10/2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya ulipo Jengo jipya la utawala, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Adv. Athuman Bamba amewata watumishi walioteuliwa kuwa maafisa waandikishaji wa Daftari la Mkazi wilayani Chunya amesema uzalendo, uadilifu na kulipenda Taifa lao kuwaongoze kutekeleza Shughuli hii muhimu
“Serikali kukuteua kufanya shughuli hii maana yake imekuamini na imeona unaweza kuifanya kazi hii kwa ubora na kwa weledi mkubwa hivyo nendeni mkatekeleze shughuli hii kwa uzalendo mkubwa maana orodha hii ni muhimu kwa mustakabali wa Jamii zetu na Taifa kwa ujumla kwani Daftari hilo la Mkazi litatumika wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa” amesema Adv. Bamba
Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu Ridhiwan Mshigati akihitimisha mafunzo hayo amewataka watumishi wote walioteuliwa kwanza kuzingatia maelekezo waliyopewa pamoja na kulinda kwa dhati kiapo walichopata Mbele ya Hakimi mkazi Mkuu Mhe James Mhanusi na kwakufanya hivyo watakuwa wameendelea kulinda Imani ya Serikali kwao kwani Serikali imewaamini kutekeleza jukumu hilo
“Mchakato wa wewe kuteuliwa kwaajili ya kazi hii umefanyika kwa hatua mbalimbali, Naomba nikujulishe haujaja hapa kwa bahati mbaya hata kidogo, Nikuombe zingatia maelekezo yote yaliyotolea hapa lakini pia fuata kanuni na miongozo mliyopewa ili zoezi liweze kukamilika vizuri na kwa wakati kulingana na miongozo ya utekelezaji wa jukumu hili muhimu” amesema Mshigati
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Chunya anawaomba wananchi wote kwamba kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura kwa mujibu wa kalenda ya matukio lakini kuwakumbusha watu wengine walioko kwenye maeneo yao kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Daftari la Mkazi la kitongoji ili upate sifa ya kupiga kura wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Halmashauri ya wilaya ya Chunya inataraji kuwa na vituo mia mbili thelasini na tatu (233) ambapo ni sawa na idadi ya vitongoji vilivyopo na imeendesha mafunzo ya Maafisa waandikishaji kwa makundi mawili ili kuwapunguzia umbali wa kusafiri maafisa hao ambapo Tarafa ya kiwanja mafunzo yamefanyika ukumbi wa Halmashauri uliopo jengo jipya la utawala wakati Tarafa ya Kipembawe Mafunzo yamefanyika Ukumbi wa mikutano uliopo shule ya Sekondari Lupa ambapo jumla ya maafisa waandikishaji 241 wakiwepo na maafisa waandikishaji wa akiba wamepata mafunzo.
Hakimu Mkazi Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe James Mhanusi akizungumza kabla ya kuwaapisha maafisa waandikishaji wa Daftari la Mkazi la vitongoji ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotaraji kufanyika Novemba 27, 2024
Maafisa waandikishaji wa Daftari la Mkazi wakiendelea kula kiapo kuonesha utayari wa kufanya kazi ya kuandaa orodha ya wapiga kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unataraji kufanyika mapema mwezi Novemba
Maafisa waandikishaji wa Daftari la Mkazi wakiendelea kupokea maelekezo na Mafunzo mbalimbali kuelekea zoazi la Uandikishaji ambapo zoezi la Uandikishaji litaanza tarehe 11-20/10/2024
Afisa Uchaguzi wa wilaya ya Chunya Ndugu Ridhan Mshigati (Aliyesimama Mbele) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya vitu wakati wa Semina ya maafisa waandikishaji wa Daftari la Mkazi la Kitongoji iliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Jengo jipya la utawala)
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.