Maafisa habari na Waandishi wa habari kutoka Mkoa wa Mbeya na Songwe wapata mafunzo ya elimu ya afya ya akili kuwawezesha kujitambua ili kuendelea kuelimisha na kuuhabarisha umma juu ya changamoto ya afya ya akili kwakuwa tafiti zinaonesha watu wengi hususani Vijana ni wahanga wa tatizo hilo pasipo wao kujua wanakabiliwa na changamoto ya afya ya akili.
Elimu hiyo juu ya afya ya akili imetolewa na Mtaalam wa saikolojia Bi Sumaiya Mahmoud tarehe 15/04/2026 kupitia shirika la DSW Tanzania linalotekeleza mradi wa Afya na Maendeleo kwa Vijana unaojulikana kama SAFA na REST katika Mikoa ya Mbeya na Songwe wakati wa kikao cha mapitio ya shughuli za mradi kilichoketi katika Ukumi wa Mikutano uliopo katika ofisi DSW Tanzanio uliopo jiji la Mbeya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la DSW Tanzania Ndugu Peter Owaga akawakumbusha Maafisa habari na Waandishi wa Habari kuhusu shirika hilo na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha maafisa hao wajibu wao katika mradi ili kuendelea kuelimisha Vijana na jamii kwa ujumla kuhusu masuala ya afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia, stadi za maisha na mambo mengine kwa maendeleo ya Taifa la leo na Kesho.
‘’Tunaendelea kukumbushana kuhusu Shirika la DSW Tanzania, shughuli zinazofanywa pamoja na miradi inayotekelezwa ili kuendelea kuaongezea uelewa zaidi kwenu ninyi kama Maafisa Habari na Waandishi wahabari kwa lengo la kufikisha elimu ya Afya na maendeleo kwa Vijana kwa wanufaika wa mradi na jamii kwa ujumla”alisema Owaga
Naye Noah Kibona Afisa Habari kutoka Wilaya ya Rungwe kwaniaba wa washiriki wengine amesema kuwa mafunzo hayo yana manufaa makubwa kwao kwani imewasaidia kkwanza kujitambua wao wenyewe lakini pia itawasaidia katika kuelimisha jamii juu ya matatizo ya afya ya akili lakini pia kupitia utekelezaji wa shughuli zamradi imewasaidia kujua wapi panapaswa kuongezwa nguvu zaidi ili kufanikisha malengo ya mradi wa Afya na Maendeleo kwa Vijana.
Kikao cha mapitio ya mradi unaotekelezwa na shirika la DSW Tanzania kimehudhuriwa na Maafisa Habari , Waandishi wa habari kuoka Mkoa wa Mbeya na Songwe , Mtaalam wa Saikolojia na Wafanyakazi wa Shirika hilo .
Mkurugenzi wa shirika la DSW Tanzania Ndugu Peter Owaga akielezea kuhusu shirila hilo kwa Maafisa habari na Waandishi wa Habari wakati wa kikao cha mapitio ya shughuli za mradi katika Ukumbi wa mikutano wa ofisi za shirika la DSW uliopo jiji la Mbeya.
Mtaalam wa Saikolojia Bi Sumaiya Mahamoud akifundisha kuhusu afya ya akili kwa Maafisa habari na Waandishi wa habari wa Mkoa wa Songwe na Mbeya wakati wa kikao cha mapitio ya shughuli za mradi.
Maafisa habari na Waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya na Songwe wakifuatilia kikao cha mapitio ya shughuli za mradi katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika ofisi za DSW Tanzania Jijini Mbeya.
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.