Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amewata wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba waliohitimu Mafunzo leo kuhakikisha wanakuwa msaada kwa jamii zao huku akiwahimiza kuendelea kulinda na kuheshimu kiapo walichokipata baada ya kuhitimu Mafunzo hayo kwani wao pia ni sehemu ya Jamii ya Tanzania wanayoenda kuitumikia baada ya kuhitimu mafunzo
Ametoa kauli hiyo leo 7.8.2025 wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Jeshi la akiba yaliyodumu kwa wiki 18 yaliyokuwa yanafanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Sangambi ambapo wahitimu themanini na Saba (87) wakiume sabini na saba (77) na wa kike wakiwa kumi (10) wamehitimu mafunzo hayo.
“Nendeni mkasaidie jamii kuleta maendeleo katika Jamii zenu mnazotoka katika kata hii ya Sangambi, Lakini pia nendeni mkaishi maisha yenye nidhamu huku mkikumbuka kwamba mmekula kiapo na kama nimesikiliza vizuri mwishoni mmesema Mwenyeezi Mungu Nisaidie, Hivyo nendeni mkaishi kulingana na kiapo hicho” Amesema Mhe Batenga
Aidha Mhe Batenga amesema amepokea changamoyo ya ukosefu wa fedha za sare kwa wahitimu wa Mafunzo huku akiahidi kwamba kwa Mafunzo yajayo Halmashauri itatenga Batenga kwaajili ya Sare na gharama nyingine zinazohitajika wakati wa Mafunzo hayo jambo litakaloongeza morali kwa vijana wengine kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Akiba
Akitoa taarifa ya mwenendo wa Mafunzo hayoMshauri wa Jeshi la akiba wilaya ya Chunya SSGT. Ngole Anderson Nkanyanga amesema jamii bado ina mtazamo hasi kuhusu jeshi hilo hivyo kupelekea washiriki wengine kukatisha mafunzo hayo kutokana na kukatishwa tamaa na jamii zao jambo ambalo sio zuri kwani jeshi hilo linalenga kutoa msaada kwa mujibu wa Sheria ya kuanzishwa kwake
Aidha SSGT Nkanyanga amewashukuru Kamati ya usalama, wadau, uongozi wa kata na vijiji na wananchi wote waliojitokeza katika hafla hiyo lakini pia kwa ushirikiano mkubwa na adhimu walioupata katika kipindi chote cha Mafunzo.
Awali akisoma Risala Mbele ya Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Chunya MG. Jonas Abel Kivinge amesema baadhi ya Changamoto ni pamoja na washiriki wa mafunzo kushindwa kumudu gharama za sare na mambo mengine pindi wawapo katika mafunzo hayo huku akipeleka ombi kwaniaba ya washiriki wengine la kupewa kipaumbele inapotokea fursa za kazi au fursa nyingine.
Mafunzo hayo yamedumu kwa wiki 18 yakihusisha washiriki mia moja na thelasini (130) lakini sababu mbalimbali zikiwepo utoro, utovu wa nidhamu na nyinginezo zimepelea washiriki waliofuzu mafunzo kupungua kufikia themanini na saba (87) wakiume wakiwa sabini na saba (77) na wakike kumi (10) pekee.
Vijana wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba kata ya Sangambi wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mhe Mbaraka Alhaji Batenga Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati wa Hafla yao ya kuhitimu mafunzo hayp
Baadhi ya Wazee maarufu wa Kata ya Sangambi wakifuatilia Hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Jeshi la Akiba kata ya Sangambi
Baadhi ya sehemu ya wananchi wa Kata ya Sangambi wafuatilia Hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa Hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Jeshi la Akila kata ya Sangambi
Kamati ya Usalama ya wilaya ya Chunya wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba kata ya Sangambi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.