Kamati ya fedha Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imewataka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupeleka bajeti zao pamoja na mapendekezo ya miradi wanayoitekeleza kwenye kamati hiyo ili kuamua kwa pamoja mradi upi uanze kuteklezwa na kwa gharama ipi mradi husika utatekelezwa kwani Madiwani ndio wanaoishi na wananchi hivyo wana uelewa mkubwa juu ya mahitaji ya wananchi wao
Maoni hayo yametolewa na wajumbe wa kamati ya fedha, uchumi na mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya mwishoni mwa juma walipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ikiwepo daraja la Lualaje linagharimu shilingi milioni mia mbili na kumi (210,116,000/=), Ujenzi wa daraja la Magunga kupitia barabara ya Ngwala linalojengwa kwa shilingi 178,214,000/= pamoja na mradi wa ujenzi wa Barabara ya Malangamilo yenye urefu wa kilomita 8 yenye thamani ya shilingi milioni 274,885,000/=
“Sasa tunaandaa bajeti ya mwaka 2024/2025 na nyinyi TARURA muwe mnatuletea bajeti yenu kwenye vikao vya kamati ya fedha ili na sisi tupate nafasi ya kushauri barabara ipi ipewe kipaumbele Zaidi lakini pia kuhakikisha bajeti inayopangwa inaenda sambamaba na uhalisia tunapoenda kukagua miradi” Alisema Mhe Mwanginde
Aidha kamati hiyo imeagiza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanafuatilia agizo la Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha barabara zinaenda kwenye maeneo ambayo miradi ya Build Better Tommorow (BBT) itatekelezwa zinafunguliwa ili kurahisisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi ili lengo la serikali la kuanzisha mradi huo litimie kama ilivyo kusudiwa
“Leo ni tarehe 12/1/2024 naomba kufikia tarehe 20/1/2024 mlete taarifa inayoonesha tayari bajeti ya kufungua barabara hizo imetengwa ili kamati hii ipate namna ya kuendelea kufuatilia utekelezaji wa suala hilo kama Mhe Rais alivyoagiza” Aliongeza Mhe Mwanginde
Akizungumza na kujibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani Chunya Mhandisi Emannuel S Kayola amesema miradi yote inaendelea vizuri lakini maoni, mapendekezo na Maelekezo ya wajumbe wameyachukua na watayafanyia kazi
Ziara ya Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya ipo katika ziara yake ya kawaida kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani Chunya na kamati imekagua miradi yenye thamani ya shilingi milioni 663,215,000/= ambayo inasimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)
Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani Chunya Mhandisi Emannuel S Kayola akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango wakati kamati hiyi ilipotembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na TARURA wilayani ya Chunya
Wajumbe wa kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango wakiendelea na zoezi la Ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na TARURA ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Pichani ni wajumbe wakikagua ujenzi wa Barabara ya Malangamilo inayojengwa urefu wa kilomita 8 kutoka Barabara kuu ya Mbeya Tabora
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.