Lengo la Viongozi wa Serikali Halmashauri ya wilaya ya Chunya wakishirikiana na wananchi wa Chunya la kuondoa Daraja la tatu katika mitihani ya Taifa liko Mbioni kufikiwa kwani kwa Matokeo ya Kidato cha Sita yaliyotangazwa tarehe 7/7/2025 Halmashauri ya wilaya ya Chunya ina wanafunzi 09 tu waliopata daraja la tatu huku wengine 441 wakiwa wamepata daraja la kwanza na la daraja la pili
Kwa ushirkiano mzuri kati ya viongozi, wadau wa maendeleo, walimu, wazazi na wanafunzi kwa ujumla wamefanikisha wanafunzi 450 waliofanya mtihani kidato cha sita kufaulu na sasa kazi kubwa inayobaki ni kuondoa daraja la tatu
Wazazi popote ulipo Tanzania Sehemu sahihi kumpeleka mtoto kwaajili ya kupata Elimu ni wilaya ya Chunya, na kwakufanya hivyo hauwezi kujutia hata kidogo
Kutazama Matokeo ya Shule ya Sekondari Kiwanja Bonyeza Kiunganishi hapo Chini
https://matokeo.necta.go.tz/results/2025/acsee/results/s1584.htm
Na Kutazama matokeo shule ya Sekondari Lupa Bonyeza Kiunganishi hapo Chini
https://matokeo.necta.go.tz/results/2025/acsee/results/s0774.htm
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.