Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Alhaji Batenga amewataka viongozi wote ndani ya wilaya ya Chunya pamoja na wananchi wegine wote kuwajali na kuwalinda wazee waliopo katika jamii zao kwa kuhakikisha wanawapatia haki zao kwani Jambo hilo lina Baraka za mwenyeezi Mungu kwa jamii na Taifa kwa ujumla
Akizungumza Mapema Oktoba 6, 2024 kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Idodoma kilichopo kwenye Kijiji cha Bitimanyangawa, kata ya Mafyeko uliolenga kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua alio pamoja na kutoa Elimu ya Umuhimu wa wananchi hao kushiriki kujiandikisha ikiwa ni hatua mojawapo kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
“Unamuonea bibi kama huyu unataka aende wapi? Hata Mungu hapendi. Viongozi tufanye kazi kwa haki lakini kwa wazee wenye umri kama bibi huyu Jamii tuwalinde kwa pamoja maana wakati mwingine wanaonewa na watoto wao hivyo jamii tuwasaidie” Amesema Mhe Batenga
Aidha Mhe Betenga amemwagiza Katibu tarafa kufika eneo hilo kufuatilia kwa kina madai ya Bibi huyo yanayoonesha Nyumba yake imeuzwa pasina yeye kujua jambo lililopelekea bibi huyo kuendelea kuishi kwenye mji wa mtu mwingine
Katika wakati mwingine Mkuu wa wilaya ya Chunya amewataka wananchi wa kitongoji cha Idodoma kuhakikisha wanashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili wachague viongozi watakao waongoza kwa kipindi cha Miaka mitano mingine na watakao msaidiia Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaletea Maendeleo katika kitongoji chao ikiwepo ukamilishaji wa Shule ambayo kwasasa ina madarasa mawili wakati madarasa mengine matatu yakiwa kiwango cha Boma, kusogeza huduma ya umeme na huduma nyingine nyingi
Ziara ya Mkuu wa Wilaya iko katika siku yake ya pili ambapo kwa tarehe 6/10/2024 Mkuu wa wilaya ya Chunya amefanya mikutano mine katika kidongoji cha Idodoma, Bitimanyanga, Kambikatoto na Kanoge huku maeneo yote akisikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu pamoja na kuhimiza wananchi hao kujiandikisha kwenye Daftari la mkazi ambapo zoezi la uandikishaji litaanza rasmi tarehe 11-20/10/2024 na kuhimitisha kwa kufanya uchaguzi Novemba 27,2024
Mkuu wa wilaya ya Chunya akizungumza jambo wakati wa mkutano na wananchi wa Kitongoji cha Idodoma kilichopo kijiji cha Bitimanyanga katika Kata ya Mafyeko. Katika Mkutano huo ndipo alipomwagiza Mwenyekiti wa Kitongoji kurudisha Shilingi laki mbii na Hamsini ambazo ilithibitika hakumrudishia Bibi aliyekuwa anamtudai Bwana Anthony
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhe Mbaraka Ahaji Batenga akizungumza na wananchi wa Bitimanyanga baada ya kusikiliza kero za wananchi wa Kitongoji cha Idodoma, alipata wasaa wa kusikiliza wananchi wa Bitimanayanga na kutatua kero zinazowakabili
Mkuu wa wilaya ya Chunya akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kambikatoto baada ya kupokea kero zao na hapo alikuwa akisimama kutoa majibu lakini pia kuwahimiza kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika uchaguzi unaotaraji kufanyika mapema mwezi Novemba
Wananchi wa Kanoge wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chunya wakati akijibu kero walizowasilisha kwake ili kupatiwa majibu wakati alipowatembelea kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.