Watendaji wa kata, waratibu wa Lishe wa kata pamoja na kamati za chakula shuleni wilayani Chunya wametakiwa kuhakikisha katika msimu huu wa mavuno Chakula cha kutosha kinakusanywa kinachoweza kukidhi mwaka mzima ili wanafunzi wawapo shuleni waendelee kupata chakula ikiwa ni mkakati wa kupambana na utapiamlo kwa watoto na kuepuka ufaulu mdogo kwa wanafunzi kwasababu ya kukosa Chakula
Akizungumza na watendaji wa kata pamoja na waratibu wa Lishe wa kata leo wakati wa Kikao cha Tathimini ya mkataba wa Lishe Robo ya tatu ya mwaka 2022/2023, Katibu tawala wilaya ya Chunya Bw Anakleti Michombero akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Chunya amesema lengo la wilaya ya Chunya ni kuongoza Kitaifa katika suala la Lishe hivyo amewataka kuhakikisha wanakusanya chakula cha kutosha kwa mwaka mzima
“Watendaji, waratibu wa Lishe shirikianeni kuhakikisha Chakula cha kutosha kwa mwaka mzima kianze kuchangishwa ili kuepuka changamoto za watoto kushindwa kupata chakula wawapo shuleni kumbukeni lengo letu ni kuongoza katika suala la lishe kitaifa”
Aidha kikao hicho kimewapongeza uongozi wa kata ya Chalangwa ambao kwa takwimu za jana Karibu gunia saba za mahindi zimeshakusanywa huku zoezi hilo likiwa linaendelea
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu. Tamim Kambona amewambia watendaji wa kata kwamba kushindwa kusimamia lishe kwenye maeneo yao ni ishara tosha kwamba kazi hiyo ya utendaji wa kata hawaiwezi hivyo hatua mbalimbali zitachuliwa dhidi ya watendaji watakaobainika kushindwa kusimamia suala la lishe ipasavyo
“Mtendaji utakayeshindwa kusimamia suala la lishe Shuleni maana yake umeshindwa kufanya kazi yako hivyo mimi nitakushughulikia ipasavyo ikiwa ni pamoja na kukuondelea majukumu haya na kumkabidhi mtu mwingine”
Wajumbe kwa nyakati mbalimbali wametoa hoja zao ikiwa ni kuweka wazi maeneo yanayoweza kuwa vikwazo katika kufanikisha zoezi hilo na baadaye kutoka na azimio moja katika kila eneo linaloonekana kuleta utata na hata kupata ufafanuzi pale palipostahili kufafanuliwa
Kiako hiki cha tathimini ya Mkataba wa lishe kilichoongozwa na Katibu tawala wilaya ya Chunya akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Chunya kimeketi leo 5/5/2023 katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) ambapo wajumbe toka kata mbalimbali yaani watendaji wa kata na waratibu wa lishe wa kata walihudhuria.
Wajumbe wa Kikao cha Tathimini ya Mkataba wa lishe wilaya ya Chunya wakiwa katika kikao cha Robo ya Tatu
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.