Katika kikao hicho waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kuuliza maswali ya papo kwa hapo na kupatiwa majibu kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Magolo M. Diwani wa kata ya Lupa aliuliza:-
Lini gari la kituo cha Afya Lupa litarejeshwa Lupa na kuendelea kutoa huduma?
Majibu: Gari hilo tayari limesharejeshwa kituoni ila dereva wa gari hilo alikuwa na matatizo ya kiafya. Mara tu baada ya matibabu atarejea kazini.
Maadhimio: Tarehe 28/10/2017 gari liwe linafanya kazi (DMO) atafute Dereva mbadala
Lini wataalamu wa zao la tumbaku mfano Bodi ya tumbaku CHUTCU watakuwepo kwenye vikao vya kisheria il kuweza kutoa majibu ya changamoto mbalimbali za zao la tumbaku kwenye vikao?
Maadhimio: CMT ijadili na kuwasilisha swala hilo ofisi ya fedha na mipango ili ijadiliwe na kuona namna wataalamu hao watakavyoweza kushiriki kwenye vikao vya kisheria ili kutoa majibu ya changamoto mbalimbali za zao la tumbaku.
Mh. Funga, diwani wa Kata ya Matwiga aliuliza juu ya
Upotevu wa maji kweye Bwawa la matwiga
Ufafanuzi: Bwawa hilo baada ya kukamilika liliachwa wazi maji yaendelee kutoka ili kupima kama maji hayo yanaweza kutoka na kutumika mwaka mzima.
Ni lini tathmini ya ujenzi wa miundombinu itakamilika katika ujenzi wa Bwawa la matwiga ili wananchi wafurahie huduma?
Majibu: Swala hilo lipo kwenye bodi ya zabuni linafanyiwa kazi
YATOKANAYO NA MUKTASARI WA 26/07/2017
a) Kila kijiji kufyatua tofali 200,000 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali
maadhimio: Baraza lijalo taarifa ya idadi ya tofali zilizofyatuliwa kwa kila kata na vijiji taarifa iwasilishwe
b) Wanafunzi wote wa kidato cha pili na nne wahamie mabwenini ili kuongeza ufaulu
-Taarifa ya maadhimio ya utekelezaji iliwasilishwa kuwa shule zote zimeshatekeleza isipokuwa Mtanila na Ifumbo
Maadhimio: Maafisa Elimu Msingi na Sekondari wafuatilie shule hizo ili kupata sababu ya shule za Ifumbo na Mtanila kutotekeleza agizo hilo.
c) Idara ya maendeleo ya Jamii kufanya tathmini ya vikundi vya kukopeshwa mikopo
maadhimio: Taarifa ya tathmini hiyo iwasilishwe kwenye kikao cha kamati ya fedha, utawala na mipango cha Novemba 2017
d). Fedha za vikao vya mamlaka makongorosi
-Taarifa iliwasilishwa kuwa fedha hizo zimeshalipwa.
Maadhimio:Fedha zote zinazotakiwa kupelekwa mamlaka ya Mji mdogo Makongolosi zipelekwe kwa wakati. Endapo hakuna fedha za vikao vya mamlaka basi hata vikao vya Halmashauri makao makuu visifanyike.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Bosco Mwanginde katika Baraza la madiwani.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndg. Damian P. Mwasiwolo akitoa salamu za Katibu tawala
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chunya Mh. Noel Chiwanga akitoa salamu za chama Tawala.
Muwakilishi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Ndg. George K. Mtasha akitoa salamu za chama chake
Waheshimiwa Madiwani ndani ya Baraza
Itigi Road
sanduku la posta: P.O box 73 Chunya
simu ya mezani: 025 2520121
simu ya mkononi: 025 2520121
Barua pepe: ded@chunyadc.go.tz
Copyright ©2017 Chunya District Council . All rights reserved.